sifa za mwanaume mwenye mapenzi ya dhat.

joyness

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2012
Posts
235
Reaction score
120
habari wana jamvi wenzangu!hizi ndo sifa za mwanaume mwenye mapenzi ya dhati kama ulikuwa hufahamu.

1. ALIYE MKWELI.
Katika hili, hekima na busara nyingi huhitajika kutumika, ngao kubwa ya utambuzi juu ya mpenzi uliyenaye kuwa mume mwema linategemea sana hili. Ukweli ni silaha muhimu sana katika uhusiano.

Japo natambua kuwa, kuna wengine watajiuliza utajuaje kama huyu ni mkweli au siyo. Kitendo cha kukutamkia kuwa, anakupenda ni cha ukweli sana hasa kama atakuwa anakupenda kwa dhati.

Cha kuzingatia hapa, anayaweka vipi maisha yake yaliyotangulia, anakueleza kwa uwazi upi hasa. Inawezekana alishawahi kuwa na uhusiano na mwanamke mwingine kabla, je amekufahamisha vipi. Chunguza kila akuambialo ili kuhakikisha ukweli wake.

Baadhi ya wanaume wanafikia hatua kuongopa na hata kuazima gari na kujifanya kuwa ni lake ili akunase. Kumbuka wahenga walisema ‘njia ya muongo ni fupi’ hivyo baada ya muda utachambua pumba na nafaka.

2. ANAYEJALI
Wahenga waliendelea kunena, `nyota njema huonekana alfajiri’. Huo ni msemo wa zamani wa wazee wetu ambao una maana kubwa sana. Kama mwanaume huyu ambaye kwa sasa ni mchumba wako (wazazi wawe wanatambua) anakupenda, lazima atakujali, hukuwazia wewe katika maisha yake yote, hukuona kuwa wewe ni mwenye thamani kubwa katika maisha yake.

Hatakusumbua kwa kutaka ngono kabla ya muda muafaka wa kufanya hivyo. Anayejali afya yako kwanza na hatathubutu kushiriki tendo la ndoa kabla hamjapima virusi vya ukimwi, anakupeleka hospitali unapokuwa mgonjwa (haijalishi kama una wazazi au wasaidizi wengine).

3. ALIYE NA MSIMAMO THABITI
Huyu huonekana mapema sana, asiyetingishika wala kushawishiwa na marafiki zake, katika mambo yasiyofaa.
Hushikilia msimamo wake katika kutekeleza yale yote aliyokuahidi na aliyopanga kuyafanya kwa ajili yenu.

Mathalani, ameambiwa na watu kuwa wewe una uhusiano na mwanaume mwingine. Mwenye msimamo huchukua muda mwingi kufanya uchunguzi juu ya aliyosikia kabla hajakuuliza chochote.

Nathubutu kusema hivyo kwa sababu kuna baadhi ya wanaume wana kasumba mbaya, wanaposikia kitu kuhusu wachumba zao, au wapenzi wao, kabla ya kufanya uchunguzi humjia juu mwanamke husika na wakati mwingine hufikia hata hatua ya kumpiga.

Hii ni hulka mbaya ambayo baadhi ya wanaume wanayo, lakini jaribu kujiuliza, kama hamjaoana anadiriki kukupiga kama ngoma na akikuoa je, si atakufanya kilema?

4. ANAYESHAURIKA
Siku zote, amekuwa mkweli kwako, anakubainishia mali zake pamoja na biashara zake. Haoni vibaya pia kukufundisha juu ya kuendesha mali zake. Inapotokea unamshauri, hukusikiliza kwa makini na kufanyia kazi ushauri unaompa. Mwanaume huyu hutulia na kuyapima maneno yako kwa makini kabla hajayafanyia kazi.

Ni vyema mumeo ashaurike (inapobidi) ili asifanye madhara mengine katika maamuzi ya familia kwa kisingizio cha ubaba ndiyo kichwa ca familia.

5. ANAYEJALI NDUGU ZAKO
Waswahili wanasema `ukipenda boga, penda na ua lake’kwa wakati mmoja, msemo huu unasisitiza upendo. Kwamba kuna vipimo kadhaa vya upendo lakini moja ni kumwangalia kama ana upendo na ndugu zako.s

Mwanaume huyu mara zote hukuulizia hali ya wazee wako pamoja na ndugu zako wengine. Hii ni sawa na mawingu kabla ya mvua. Kwa sababu kama atashindwa kuwajali ndugu zako japo kwa kuwajulia hali utakapoingia katika ndoa atakuruhusu ukawasabahi kweli?
 
Namba 4...
Nimeshuhudia ubinafsi wa wanawake wengi hapa JF, haswa linapokuja suala la fedha. Hii imenipa mwangaza wa kubaini uchoyo kama sio ulimbukeni walionao jinsia KE linapokuja suala la fedha, sasa naomba nikuombe mleta thread hii, tafadhali, hebu shawishi wanajamvi kutetea hicho kipengele namba nne.
 

Huwa wanasema chao ni chao cha mwanaume ni cha familia
 
Sifa zote ninazo ila sasa sioni wa kuwa karibu nae wote ni head ache tu
 
Kama na wewe mwanamke utakuwa na sifa kama hizo basi mahusiano yatakuwa bora, sio hivyo vitu viwe upande mmoja
 
samahani nadhani sijakupata vizuri wabinafsi kivipi?
 
Kumbe jibu unalo.

Sasa mnafanya kazi ya nini wakati mnawageuza wanaume kama kwa kuwanyonya, unakuta mwanaume amekondeana balaa alafu mwanamke amafumuka balaa
 
Huwa wanasema chao ni chao cha mwanaume ni cha familia

Hapana si wote! mi ninachojua wanawake wengi katika ndoa ni chachu ya mafanikio, sasa iweje wewe ufiche chako halafu cha mwanaume kiwe cha wote! hiyo ni tabia tu ya mtu kuwa mbinafsi! au ndiyo wale wanaokaa mguu mmoja nje mwingine ndani!

Lakini kwa mwanamke yeyote ambaye miguu yote iko ndani hawezi kuwa hivyo; Japo kiukweli mwanaume ndo anayetakiwa kuwa kinara wa kumudu familia mwanamke anachangia tu!

Japo kusema kweli mwanamke asilimia kubwa la pato lake linaingia katika mahitaji ya kifamilia kwani mwanamke ndo mwangalizi mambo mengi ili maisha yaende inawezekana akawa hamwonyeshi mwanaume kipato chote lakini kinaishia kwenye mambo kama mavazi ya familia(baba na watoto), vyombo, mapambo, n.k

Kikubwa kunapokuwa mapenzi ya kweli/dhati huwezi kuona kipi cha nani bali wote mtaungana ili muweze kufikia malengo mliojipangia! tofauti zinakuja kama hakuna upendo au kuna kaubinafsi mmojawapo kaonyesha, au kuna ufujaji wa pesa kwa mmojawenu.
 
sio fair jamani hicho chenu mnahonga viserengeti boy?

hamna bna,mwanamke mwenye akili kwao ana mjengo wa maana,biashara ya maana na mume haijui,mwanamke anaehonga mwanaume ni mjinga na hajitambui!
 
tatizo wanaume hamkawii kubadilika,mnafanya vitu vya maendeleo pamoja, mwisho wa siku unakua c mali kitu kwake,inabidi wadada tuishi kwa akili tu,chetu chetu ,chao chetu ndio formula ya ndoa!
 
hao wanaume wamekaa kinadharia mno. most men are insecure/hawajitambui/unsettled. kama unatafuta someone mwenye hizo sifa tegemea kusubiri muda mrefu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…