Mkuu sio vizuri kukatisha watu tamaa. Hebu unesha wapi alikuwa anaenda vizuri akaharibu?
Ushauri wangu sasa.
Kwanza ni seme kijana amekidhi vigezo vya kwenda A level tena bahati nzuri sayansi. Muongozo wa wizara unasema ili mwanafunzi aruhusiwe kwenda A level (iwe gvt au prvt) anatakiwa asipate GPA chini ya 1.6 au kwenye tahasusi(combi) apate kuanzia C na kuendelea. Hivyo kama mwanafunzi amepata C tatu za ndani ya kombi GPA haiangaliwi tena.
Kwa maeelezo hayo dogo kafaulu PCB so hapo anakwenda bila shida kabisa. Kuhusu shule ya gharama nafuu sio rahisi kusema ni ipi. Ila kama lengo ni kumsaidia dogo haswa kwenue kombi ya sayansi mpeleke shule nzuri. Moshi kuna shule nzuri kama MAJENGO SECONDARY na Ada yake ni kama 1.2 hivi kwa mwaka ila ni shule ya kutwa. Hosteli zipo ila haziendeshwi na shule na ada ya hosteli ni kama laki 8 hivi kwa mwaka. Hapo dogo akiwa sirius anapiga mkuu.