Iwapo tu kiwango chake kitakuwa kama cha jana au zaidi kwa msimu mzima na iwapo atajirekebisha nidhamu yake ndani na nje ya uwanja Simba wafikirie kumrudisha huyu mwamba. Uwezo wa Tairone Santos na Kennedy Juma wanasubiri sana kwa huyo Nyoso. Na haitakuwa ajabu kwake kurudi kama viongozi wataona anafaa kurudi kwani kwa siku za karibuni wamerudi Miraji "Sheva" na Shamte. Yote kwa yote viongozi ndio wanaojua mahitaji ya timu na ndio wenye dhamana ya timu na maamuzi ya mwisho nani asajiliwe nani asisajiliwe sisi wengine ni kutoa maoni yetu tu na kusubiri kuona burudani uwanjaniKwa iyo mnapendekeza arudishwe msimbazi!