Habar za leo ndugu wanajukwaa,
Kwenye mada moja kwa moja;sote tunaoamini tunafaham kuwa shetani alikuwa ni malaika wa sifa huko mbinguni (alikuwa muimbaji) baadae alipotaka kuichukua nafasi ya Mungu ndipo Mungu alipokasirika na kuamua kumtupa kuzimu
Shetani alipofika kuzimu akaanza kufanya kazi kijanja na kwaakili nyingi sana kwa kupandkiza vipaji vibaya kwa wanadamu,mfano wa vipaji anavyowapandkizia wanadamu ni pamoja na hivi;
1.Uongo
2.Usinzi
4.Ulevi
5.Ulafi (ikiwa ni pamoja na kutaka kumiliki vitu vingi pekee yako)
6.Usingiziaji
7.Hasira
8.kutokusamehe
9.Kutukana
10.Ugomvi
11.Kutokutaka suluhu
12.Kutokuwapenda watu bila sababu za msingi
13.Kuwashuhudia watu uongo
Nb:kila mwanadamu kuna mahali shetani amempa kitengo,hakuna mwanadamu ambaye shetani hajampa kitengo
Swali la msingi;je,wewe shetani amekupa kitengo gani ili tuanze kuombeana kuanzia hivi sasa?