Ripota wa
AyoTV na
millardayo.com wakati akiwa anasubiria mchezo wa fainali na mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu wa michuano ya mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 maarufu kama
AFCON U-17, amekusogezea mambo matano usiyoyafahamu kutoka
Gabon.
1- Wote tumekuwa tukiamini au kuzoea kuona kuwa Taxi za Airport ni gari ambazo nzuri na wakati mwingine zinakuwa hata mpya husani kwa
Tanzania kutokana na kuwa zinakuwa sehemu ambayo wageni kutoka nje ya nchini wanaingia, hiyo ni tofauti kwa
Gabon Taxi nyingi au gari zinazobeba abiria
Gabon ni chakavu na gari mpya za watu binafsi.
Taxi za Airport Libreville
2- Kila nchi ukifika kama ni mpenzi wa muziki basi utatamani kufahamu msanii au wimbo wa msanii mkali wa nchi husika, kwa nchi ya
Gabon msanii maarufu ni mama wa Rais wa sasa wa
Gabon Patience Dabany ambaye alikuwa ni mke wa Rais wa zamani wa
Gabon mzee
Omar Bongo Ondimba.
3-
Gabon ni nchi ambayo ina idadi ndogo ya watu milioni 1.8 ukilinganisha na
Tanzania ambayo ni nchi yenye watu zaidi ya milioni 40, mji mkuu wa nchi hiyo ambao unajulikana kama
Libreville ni mji ambao unajumla ya watu 578156 hiyo kwa mujibu wa takwimu 2017.
4- Kwa nchi ya
Gabon wenye wanasema msichana yaani mwanafunzi akipata ujauzito wakati bado yupo shuleni hawezi kufukuzwa shule bali ataruhusiwa kuendelea na masomo huku akiwa bado mjamzito akikaribia kujifungua anapewa ruhusa ya uzazi na baadae anarudi kuendelea na masomo.
5- Staa wa soka mkubwa Gabon ni nahodha wao
Pierre-Emerick Aubameyang ambaye anacheza
Borussia Dortmund licha ya kuwa na jina kubwa
Gabon hana makazi yaani huwa anakuja timu ya taifa na kuondoka, hiyo inatokana na kuzaliwa na kukulia
Ufaransa, baba yake ana asili ya
Gabon na mama yake ni mfaransa mwenye asili ya Hispania.
Unaweza kutazama mahojiano ya Mkurugenzi wa SportPesa na AyoTV baada ya kuingia mkataba.