Shamba/Kiwanja Dodoma!

Shamba/Kiwanja Dodoma!

Bukijo

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2010
Posts
208
Reaction score
71
Kuna mashamba yanauzwa Dodoma eneo linaitwa NTYUKA km 5 toka Dodoma mjini upande wa Kusini-Mashariki mwa Dodoma barabara ya kuelekea MVUMI mission.

Kata ya Ntyuka imepakana na Chuo kikuu cha Dodoma upande wa mashariki ni karibu na Hospitali moja mashuhuri sana hapa Dodoma inaitwa DCMC. Kuliona eneo hili waweza kugoogle kwa key word-NTYUKA au fungua Tovuti ya UDOM utaona raman nzima ya NTYUKA.

Mashamba yanauzwa bei tofauti tofauti kulingana na ukubwa wa eneo,wenyeji huuza kwa bei za kawaida sana kulingana na mahitaji ya muuzaji na mnunuzi.

Kwa eneo dogo kabisa la 30X30M unawezapata kwa 2M na ekari moja unawezapata kwa 6M ila bei haitabiliki vizuri maana ni makubaliano na muuzaji.

System ya maji na umeme ipo pia gharama za ujenzi ni nafuu sana kwani Roli la mchanga ni kati ya Tsh45,000-55,000 roli la mawe kati ya 70,000 had 85,000 kokoto 120,000-150000 hivyo kama ukijipanga unaweza nunua na kujenga nyumba ya kawaida kwa gharama nafuu sana.

Kama utapenda kujichukulia eneo waweza wasiliana nami nikuunganishe na wenye mashamba,sifanyi udalali wala biashara ila nimependa kuwashirikisha wale wenye kuhitaji.Kwa maelekezo zaidi waweza kini-PM kama uko serious.


Angalizo:
Eneo halijipimwa na mamlaka ya ustawishaji makao makuu CDA hivyo bado liko chini ya Serikali ya Kijiji.Ila ni sehemu salama na linakua kwa haraka sana miundo mbinu yote ipo.
 
Kama alijapimwa na ukajenga kabla alijapumwa si unatafuta kuvunjiwa
 
Huku Dodoma hatar watu wanachomwa moto wakizaniwa wa nyonya DAMU SASA UKIJENGA NYUMBA KUBWA HUKO OUT OF TOWN SIWATAJUA SEHEMU YA KUNYONYEA DAMU huko Dom baado sn
 
Kama alijapimwa na ukajenga kabla alijapumwa si unatafuta kuvunjiwa
Ni kijijini kuna wenyeji wengi so sio pori wazawa ndo wanapunguza maeneo yao kwa kuuza kwahiyo si dhani kama kuna utaratibu wa kuvunjiana nyumba kama unavyodhani wewe!
 
Km 5 toka mjini halafu hapajapimwa? Hebu ongea vizuri mkuu, is this genuine? imekuwaje CDA hawajapima km 5 toka mjini? maana unaweza kununua kumbe ni eneo la stendi kuu
 
Huku Dodoma hatar watu wanachomwa moto wakizaniwa wa nyonya DAMU SASA UKIJENGA NYUMBA KUBWA HUKO OUT OF TOWN SIWATAJUA SEHEMU YA KUNYONYEA DAMU huko Dom baado sn
5km from town sio out of TOWN we ulizia kunamtaa mmoja unaitwa wa Maprofessa yaan ukifika utashangaa nyumba za uhakika na wakazi wa pale ni Maprof wa UDOM,St.John's,Mipango n.k kwahiyo sio porin kama huko kwingine unakosikiaga
 
Km 5 toka mjini halafu hapajapimwa? Hebu ongea vizuri mkuu, is this genuine? imekuwaje CDA hawajapima km 5 toka mjini? maana unaweza kununua kumbe ni eneo la stendi kuu
Hakujapimwa ndio had kuna eneo linaitwa makulu 3km toka town njia ya kwenda UDOM karb office za Hazina/BOT na Ukumbi wa CCM hakujapimwa nako pia usishangae hawa CDA wanapenda maeneo ya wazi zaid kuliko yale yanayokaliwa na wenyeji toka zaman.Wanapima nahisi kutokana na interest zao
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom