Shaka Hamdu Shaka ana hatari huyo

AFRIKAMOJA

Member
Joined
Aug 11, 2022
Posts
30
Reaction score
37
Ziara za mwenezi Shaka zinakuwa za moto sana maana anaeleza kazi kubwa anayoifanya Rais Samia Suluhu Hassan kwa wananchi.

Anasikiliza kero na kuhakikisha wahusika wanatoa majibu halisia...wakibabaisha chama kinatoa mwelekeo au ushauri kwa serikali...balaa zaidi anajishusha na kujichanganya na wananchi wa kawaida kabisa hii ni siasa kubwa sana.

Hakika haya yote yanakipa Chama cha Mapinduzi hamasa kubwa kwa umma na kuwapa wananchi matumaini na imani zaidi kwa chama na serikali yao...piga kazi mwenezi wetu kwani huo ndio uenezi.

 
Hana jipya zaidi ya kutafuta perdiem tu huyo... ameshaachana na Joho wa Mombassa?
 
Shaka ni mtu na nusu, kazi nzuri Sana
 
Hao wanachama wanapelekwa kwenye hiyo mikutano kama mzigo,hamna Mtanzania kutoka bara anamkubali Mzanzibari-hakuna hata mmoja.
 
CC ya CCM nayo sijui huwa wanafikiria kwa kutumia nini,yani unampaje Mzanzibar nafasi ya uenezi huku Wanachama wako 99% ni Wabara-strategy mbovu kabisa.
 
Tatizo la Mtanzania Khanga,Tishet,Kofia anasahau madhila yote na kuanza kukata kiuno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…