Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndg Shaka Hamdu Shaka leo Jumamosi tarehe 01 Oktoba, 2022 amekuwa sehemu ya mamia ya washiriki katika mbio za NMB zilizofanyika viwanja vya Leaders Kinondoni, Dar es Salaam.
Kauli mbiu katika mbio hizi ilikuwa 'Mwendo wa Upendo' zilizolenga kuchangisha fedha kwa ajili ya matibabu ya Fistula kwa wanawake wenye tatizo hilo kupitia CCBRT.
Mgeni rasmi katika mbio hizi alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa ambapo amefanikisha kuchangishwa kwa shilingi millioni 600 kwa ajili matibabu ya wanawake wenye matatizo ya Fistula.