Shairi la mapenzi

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,539
Reaction score
4,852
1. Wewe ndie nyota yangu,usiku wamulikia.
Uniachi peke yangu,ukanacha ninalia.
Nikabaki peke yangu,mbali ukanikimbia.
Nakupenda ewe wangu,kwengine siwezi kwenda.

2. Wewe ndie mwezi wangu,usiku waangazia.
Ewe ndie taa yangu,mwanga wanimulikia.
Wewe ndie nuru yangu,wewe ndo langu pazia.
Nakupenda ewe wangu,kwengine siwezi kwenda.

3. Wewe ni asali wangu,nyuki sitowafukuza.
Kuvunja mzinga wangu,ni jambo nisiloweza.
Nikabaki peke yangu,ulimwengu kuniweza.
Nakupenda ewe wangu,kwengine siwezi kwenda.

4. Ewe ndio shuka langu,lanilinda kwa baridi.
Wewe ndie koti langu,daima sitokaidi.
Takulinda vazi langu,ili nije kufaidi.
Nakupenda ewe wangu,kwengine siwezi kwenda.

Maoni,ushauri=iddyallyninga@Gmail.com
 
Kwenye bluu::kwa wataalam wa lugha adhimu ya kiswahili...hiyo ndio lugha ya ushairi au...
Msaada kwenye tuta tafadhaliiii
::::
Btw, asante kwa tungo nzuri

 
Sawa,inaweza kuwa sehemu pia ya kuelimishana kuhusu lugha yetu ya kiswahili.
Kuwa huru (SI UNIT) hasa pale utapoona panamapungufu ili turekebishane na hiyo itapelekea wengi kuendelea kudumisha lugha yetu.
Usiogope na ndio maana nimetoa email yangu ili tupeane vitu vingi vya msingi.
Pamoja tunaweza kudumisha lugha yetu,kazi njema.
 
Last edited by a moderator:
Twende kazi MO11 ili shairi liongezeke urefu.
Kazi njema.
 
Watu munawaza mapenzi, wakati dunia imekwisha**

Achana na mawazo ya kipuuzi, watu tunahagaika na maisha**
 
NI SEHEMU TU YA KUENDELEZA FANI YA USHAIRI NA UNAWEZA UKAPATA MASHAIRI YASOKUWA YA MAPENZI KAMA LA "kufuli,nasra mvungi,meja khatibu,katiba mpya nakadhalika "
UNAWEZA PIA KUSOMA SHAIRI HILI NA KUTOA MAONI.
> > > > > > >.
AJALI BARABARANI,TWAWEZA KUZIEPUKA.
ROHO ZISIWE REHANI,UHAI UKATUTOKA.
TUKAWA SI MASHAKANI,KWA KUPETUKA MIPAKA.
MAAMUZI KUCHUKUA,AJALI TUTAEPUKA.
2>MIKASA BARABARANI,WENGI WETU TWAITAKA.
TUWAPO NDANI GARINI,BALAA TUTAEPUKA.
TUTAPOKUWA MAKINI,HATUTOWEZA SUMBUKA.
MAAMUZI KUCHUKUA,AJALI TUTAEPUKA.
3>ABIRIA NAMBA WANI,DEREVA KUMUONGOZA.
UNAPOKUWA NJIANI,ASIJE KUTUCHUKIZA.
UKAWA WE HATARINI,KWAKOGOPA KUMBEZA.
MAAMUZI KUCHUKUA,AJALI KUZIEPUKA.
4>UPITAPO DARAJANI,USIJE KUOVATEKI.
UKANGIA LAWAMANI,GEREZA LIKAWA HAKI.
WATOTO WAKO NYUMBANI,WAKAWA NA NYINGI DHIKI.
MAAMUZI KUCHUKUA,AJALI KUZIEPUKA.
5>UTAENDA KABURINI,KANUNI USIPOCHUNGA.
TUTAIMBA BURIANI,MAUTI YAKIKUFUNGA.
BORA SANA UMAKINI,USULI USIJEPINGA.
MAAMUZI KUCHUKUA,AJALI KUZIEPUKA.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…