Watawala watambue, kilio wakisikie Ukasuku waambae, waikatae ya kale Machakato uenee, na demokrasi ikue Katiba ya wananchi, nauliza tutapata?
Kukaa peke Dodoma,kuichambua rasimu Kilio cha kina mama, haki zao ni adimu Ile siku ya kiama, waso haki ni dhalimu Katiba ya wananchi, nauliza tutapata?
Beti tano nakomea, kalamu naweka chini Katiba kuongelea,sitachoka ulimini Tunataka ya kumea, iuondoe uduni Katiba ya wananchi,nauliza tutapata?