Shairi: Heko mjaza ukurasa

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,539
Reaction score
4,855
HEKO MJAZA KURASA.

1)ole adharau mwiba,atapata maumivu.
Ndogo hujaza kibaba,kubwa hushiba mashavu.
Penati wameikaba,na kuzisahau nyavu.
Heko mjaza kurasa,kwa kuwashinda magwiji.

2)fani hitaki madevu,wala gongo lilopinda.
Yataka fikra angavu,siyo kale zilokonda.
Bora umeona nyavu,acha wacheze mnanda
Heko mjaza kurasa,kwa kuwashinda magwiji.

3)jina hili ni utani,hapa limeja tumika.
Umebeba hii fani,kwenye kata wasikika.
Chukua yako medani,fani izidi panuka.
Heko mjaza kurasa,kwa kuwashinda magwiji.
HA HA HA HA HA HA.

Shairi=HEKO MJAZA KURASA.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010160.
iddyallyninga@gmail.com
 
na kweli heko amejaza kurasa na amewashinda magwiji
 
ha ha ha ha ha KENZY ,kumbe nawe unaelewa hadi tungo kama hizi.
duuuh heko kwako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…