Habari za leo. Karibu Jf
Umesema vyema.
Ili serikali iweze kuwasaidia wakulima hawa wadogo wadogo ni muhimu sana waungane na kuwa na umoja wao.
Kwa uzoefu wangu ni rahisi serikali kuwasaidia wakulima wakubwa. Kwa kuwa tayari hao wanatambulika.
Wakulima wadogo wadogo wakijiunga wanaweza kusaidiwa na serikali na taasisi nyinginezo maana inakuwa rahisi kupewa mafunzo, kununua pembejeo kwa ujumla na kupunguza bei. Kupata zana za kilimo kwa bei nzuri. Mf matrekta, ambayo yataweza kuwasaidia. Kutafuta masoko kwa pamoja na faida nyingine nyingi.
Faida nyingine ni kukutana na wote wenye changamoto za iana moja na kuzitafutia ufumbuzi. Maana wataweza kuchangia mawazo na kupata namna ya kujikwamua.