Serikali iwaache wanawake wajiuze?

Djunior

Member
Joined
Sep 28, 2010
Posts
45
Reaction score
1
Wapendwa wanajamii, naleta kwenu malalamiko yangu kwa masikitiko makubwa, kuhusu hawa dada zetu wanaojiuza nyakati za usiku. Upelelezi wangu umekamilika ndio maana naleta hoja,hapa Tanga nimejaribu kumhoji dada mmoja ambaye hujishuhulisha na kazi hiyo. Na nilipo muuliza kwa nini anajiuza kwanza alisema kutokana na ugumu wa maisha na pili alielekeza kiliochake kwa serikali kuwa haiwajali na Mh Kikwete alitoa fungu la pesa lililoitwa tajirika na Kikwete pesa za mkopo matokeo yake ziliishia kwa wakinamama wenye uweza na wao kubaki bila kitu. Akasema wanaomba kama serikali imeshindwa kuwapa mikopo nafuu iwaruhusu kufanya kazi yao ya kujiuza. Kwenu wanajamii, tuishauri nini serikali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…