Habari za weend wana jf wote,
Binafsi nashindwa kuelewa kuhusu sifa zinazotumika kutoa ajira mpya kwa walimu wakufundisha shule za sekondari maana wapo wengi wameachwa mtaani bila ajira eti kwa kigezo cha kwamba wamesomea kufundisha somo moja kwa wao siyo walimu.sasa kuna haja gani ya serikali kuendelea kuwagharamikia watu wasio kuwa na tija kwa taifa letu? na je kuna haja ya serikali kuendelea kulialia upungufu wa walimu wakati wamewaacha bila kuwaajiri? Naomba serikali itoe tamko kwamba haina uhaba wa walimu tena ili tujue kwamba sasa hakuna haja kusomea fani hii ya ualimu.
Nawasilisha
Pole sna, ila uelewa wangu serikal inagharamia elim yako c kwa ajiri uje uajiriwe bali ni kuelimisha taifa lake na kuweza kujikomboa kutokana na mazingira husika, pili asahiv serikal ina walimu wa kutosha ila changamoto iliyopo na kuwa walimu hawapo equal distributed kutokana na mahitaji, nadhan nmesomeka mzee wa Bed!