Kati ya mambo yanayochelewesha maendeleo ya watu au taasisi binafsi zinazonuia kutoa huduma vijijini kwa wananchi pale ambapo kuna mahitaji ni kukosekana kwa miundombinu kiunganishi kati ya serikali kuu na serikali za mitaa. Kwenye ngazi ya kata kuna viongozi wanaoitwa wenyeviti wa vitongoji au kijiji ambao nagundua kuwa wao kazi yao ni kuonyesha njia na kuhamasisha.Katika ngazi hiyo hiyo ya kata kuna watendaji ambao wanatekeleza sera zilizowekwa na serikali iliyoko madarakani,hapa kuna watendaji wa kitongoji au kijiji ambao hadi leo najitahidi kujua kama wanateuliwa au wanaajiriwa kwa nafasi hizo.Watendaji katika ngazi ya kata ikiwa ni pamoja na jopo zima la watumishi wa halimashauri wana aina yao ya uongozi au utendaji ambao mimi binafsi nimeshindwa kuuelewa maana mara nyingi hawataki kuhimizwa kufanya kazi ambayo wanawajibika nayo, labda kwa kuwa hawasimamiwi na mtu au kwa kuwa wana mamlaka kamili na hawapaswi kusimamiwa na mtu mwingine isipokuwa wakurugenzi wa halimashauri.Kwa kuwa JF kuna hazina kubwa ya michango ya mawazo ningeomba wale wanaofahamu vizuri muundo na utendaji wa vyombo hivi viwili wanipe darasa ili nami niweze kuelimika kwenye hili. Nimeanza mada hii kwa kutoa angalizo la ucheleweshaji wa maendeleo ya watu kwa kuwa ndivyo ninavyodhani,ninapotafakari jinsi mambo yanavyoendeshwa ngazi za chini za utawala.Huo ni mtazamo wangu ambao yawezekana siyo sahihi na niko tayari kukosolewa.Natanguliza shukurani,
Mkuu kwanza kabisa kuhusu hao watendaji wa vijiji/ kata ni wajiriwa wa serikali na nafsi zao hutangazwa na hufanyiwa usaili na kuajiliwa utumishi wa umma zamani ilikuwa kuanzia elimu ya form four lakini siku hizi lazima wazie elimu ya cheti, stashahada, shahada ktk fani za utawala , sociology , na kadhalika ila kwenye ngazi ya cheti na diploma wana chuo chao cha Serikali za mitaa Homboro- Dodoma , watendaji wa kijiji/ kata wapo chini ya mkurugenzi ( TAMISEMI) .Kati ya mambo yanayochelewesha maendeleo ya watu au taasisi binafsi zinazonuia kutoa huduma vijijini kwa wananchi pale ambapo kuna mahitaji ni kukosekana kwa miundombinu kiunganishi kati ya serikali kuu na serikali za mitaa. Kwenye ngazi ya kata kuna viongozi wanaoitwa wenyeviti wa vitongoji au kijiji ambao nagundua kuwa wao kazi yao ni kuonyesha njia na kuhamasisha.Katika ngazi hiyo hiyo ya kata kuna watendaji ambao wanatekeleza sera zilizowekwa na serikali iliyoko madarakani,hapa kuna watendaji wa kitongoji au kijiji ambao hadi leo najitahidi kujua kama wanateuliwa au wanaajiriwa kwa nafasi hizo.Watendaji katika ngazi ya kata ikiwa ni pamoja na jopo zima la watumishi wa halimashauri wana aina yao ya uongozi au utendaji ambao mimi binafsi nimeshindwa kuuelewa maana mara nyingi hawataki kuhimizwa kufanya kazi ambayo wanawajibika nayo, labda kwa kuwa hawasimamiwi na mtu au kwa kuwa wana mamlaka kamili na hawapaswi kusimamiwa na mtu mwingine isipokuwa wakurugenzi wa halimashauri.Kwa kuwa JF kuna hazina kubwa ya michango ya mawazo ningeomba wale wanaofahamu vizuri muundo na utendaji wa vyombo hivi viwili wanipe darasa ili nami niweze kuelimika kwenye hili. Nimeanza mada hii kwa kutoa angalizo la ucheleweshaji wa maendeleo ya watu kwa kuwa ndivyo ninavyodhani,ninapotafakari jinsi mambo yanavyoendeshwa ngazi za chini za utawala.Huo ni mtazamo wangu ambao yawezekana siyo sahihi na niko tayari kukosolewa.Natanguliza shukurani,
Asante sana mkuu, naomba nije inbox unifundishe huu muundo natamani kuujua kiundani zaidiMkuu kwanza kabisa kuhusu hao watendaji wa vijiji/ kata ni wajiriwa wa serikali na nafsi zao hutangazwa na hufanyiwa usaili na kuajiliwa utumishi wa umma zamani ilikuwa kuanzia elimu ya form four lakini siku hizi lazima wazie elimu ya cheti, stashahada, shahada ktk fani za utawala , sociology , na kadhalika ila kwenye ngazi ya cheti na diploma wana chuo chao cha Serikali za mitaa Homboro- Dodoma , watendaji wa kijiji/ kata wapo chini ya mkurugenzi ( TAMISEMI) .
Kuhusu muundo huu wa Tamisemi ngazi za chini
1. Kijiji. a) mtendaji wa kijiji ni katibu/ mtendaji/msemaji wa mambo yote yanayohusu serikali ktk ngazi ya kijiji, ni katibu wa mwenyekiti wa kijiji
Mwenyekiti wa kijiji pamoja wa wenyeviti wote vitongoji ndio wana unda serikali ya kijiji hivyo mambo yote yanayohusu maendeleo ya kjiji kweye vikao vyao ndiyo yanaratibiwa na mtendaji wa kijiji na huyatolea mhutasari na kuupeleka kwa mtendaji wa kata au moja kwa moja kwa Mkurugenzi mtendaji (W) pia ngazi hii ina institution ( taasisi) kama shule za msingi/ Secondary, zahanati, idara za kilimo/ mifugo , afya e.t.c hizo zote huandaa bajeti ya kijiji na kuipeleka kwenye kikao cha WDC pamoja na kutekeleza maagizo kutoka juu na kusolve matatizo kijijini.
2. Kata huundwa na Diwani, mtendaji wa kata pamoja na watumishi wote wa aerikali ngazi ya kata kama maafisa kilimo/ mifugo, mratibu elimu kata, afisa mendeleo jamii, afisa afya.
Diwani ni mwenyekiti wa W. D .C na wajumbe wake ni wenyeviti wa vijiji vyote vinavyo unda kata , mtendaji kata ndio katibu wa kikao hicho pamoja wataalamu wote katani ndio hushauli kikao hicho pamoja na kujadili bajeti ya kata nzima na kuituma kwenye full concel ( kikao cha madiwani wilayani)
Hivyo serikali za mitaa ndizo zinazotekereza maagizo yote yanayotolewa na serikali kuu na zinatoa huduma kwa wananchi kwa niaba ya serikali kuu
Baraza la Madiwani mtendaji wake ni mkurugenzi ambayo ni karibu wa kikao na mtekelezani/msimamizi wa utekelezaji.Asante sana kwa elimu nzuri, swali langu Je, mtendaji anaruhusiwa kuingia kwenye baraza la madiwani?
Mmh! Siyo katibu tawala?? Tarafa ziko nyingi Sana ktk mkoa.Pia kimkoa Kuna katibu wa Tarafa.