Serengeti: CCM yajifukia kaburini

don-oba

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2011
Posts
1,388
Reaction score
683
Jana nimesoma gazeti la Mtanzania likiandika kwamba viongozi wa CCM wilaya ya Serengeti wamtembelea Mh Lowasa nyumbani kwake, kumshawishi achukue fomu ya uraisi 2015. Viongozi hao wakiongozwa na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Serengeti ndg Vicent Nyamasagi na mwenyekiti wa halmashauri ndg John Ng'oina.

Mtakumbuka katika uchaguzi serikali za mitaa uliopita CCM imegaragazwa vibaya maeneo mengi kutokana na uongozi mbovu wa mwenyekiti huyu. Viongozi hawa ndio waliomgharimu mkurugenzi wa wilaya kufukuzwa kazi kutokana na kasoro nyingi zilizojitokeza ikiwa ni pamoja na uchaguzi kuhairishwa.

Mwenyeketi huyu wa CCM anatembea kifua mbele na kujitapa kwamba endapo Lowasa akishika dola atateuliwa kuwa mkuu wa wilaya. Kijiji anachotoka kiongozi huyu CHADEMA ndio inaongoza, mtaa anaotoka mbunge wa Serengeti mh Kebwe CHADEMA inaongoza, vijiji wanavyotoka mwenyekiti na makamu wake halmashauri vyote viko UKAWA.

Hadi sasa CCM haijui itamsimamisha nani kiti cha ubunge kutokana na kwamba wananchi wengi hawamtaki mbunge anayemalizia kipindi chake Mh Kebwe na yeye mwenyewe analijua hilo na inasemekana hatagombea kwa awamu nyingine tena. Mbunge huyu amebaki kuwa mkazi wa Dar es salaam na tangu uchaguzi ulivyoisha mwaka 2010 ni nadra sana kumwona jimboni kwake.

Kuanguka na kufa kwa CCM wilaya ya Serengeti kumesimamiwa madhubuti na mwenyekiti wao ndg Vicent Nyamasagi akishirikiana na wasaidizi wake John Ng'oina ambaye ni mwenyekiti wa halmashauri pamoja na mbumbumbu mmoja asiyejua kusoma wala kuandika ndg Jumanne Kwiro ambaye ni makamo mwenyekiti wa halmashauri. Ila kutokana na ushawishi wao kifedha wamepewa madaraka makubwa ndani ya CCM.

Tayari UKAWA wana upepo mzuri jimbo la Serengeti, baadhi ya wagombea zaidi ya watano wamepiga kambi jimboni hapa kushawishi watu wawachague.
=========================

Chanzo:Mtanzania
 


Kebwe asahau ubunge Serengeti, na huyo bwana mdogo Vicent ni mchumia tumbo tu.
 
Mbona sifa kubwa ya ufisadi aliyonayo hawajaisema?.
Kama kungekuwa na simu za kuwasiliana na wafu, tungempigia Nyerere kumjulisha sifa alizopewa Lowasa na viongozi wa ccm Serengeti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…