Kumbe rais wa Senegal naye ni kibaraka wa nchi za magharibi? hivi kweli afrika kwa mwendo huu tutafika kweli? Kutumia siraha kupambana na serikali iliyopo madarakani ni demokrasia? Hivi hayo yanayotokea libya yakitokea kwake ataita hiyo ni demokrasia na atakuwa tayari kuachia madaraka? Ni kiongozi gani katika afrika ambaye ameweza kutumia raslimali za nchi yake kwa manufaa ya nchi na watu wake kama sio ghadafi? tuacheni unafiki afrika, demokrasia gani wakati watu wanakufa kwa njaa na magonjwa kutokana na umaskini? si bora gadafi kukaa kwake muda mrefu madarakani kwa faida?