Second Round Admission: Vyuo vingine vimewaibia wanafunzi walioomba

KIFPA

Member
Joined
Oct 3, 2012
Posts
64
Reaction score
18
Jamani wan Jamvi, napenda kuwashirikisha masikitiko yangu kwa hiki kilichotokea kwenye 2nd round admision ya vyuo vikuu na nitatoa mfano wa chuo kimoja.

Jumapili nilijisajili CUHAS na kabla ya kuendelea nililazimika kufanya malipo kwanza. Jana nilifanya malipo na katika kufanya malipo nilikutana na wenzangu wengine nao wakilipia.

Baada ya kuatach bank pay-in-slip system ikatujulisha kuwa tusubiri activation email kwenye email zetu ndani ya masaa 24 ili tuendelee kuchagua kozi tunazotaka.

Leo naamka naangalia email sijaona mpaka sasa na kibaya zaidi ile page ya kulog in imeandikwa admision closed (unaweza hakiki)

Nimewapigia simu kwa namba walizotoa hawapokei maana nilitaka niwaulize mbona wamefunga admision mapema tofauti na tangazo lao lilivyosema?(lilisema tarehe10/10/2017) maana siku haijaisha

Ombi kwenu wadau naomba mnishauri nifanye nini wakati vi hela vyangu 30,000 nilivyoomboea niliomba kwa mtu wamevichukua.

Licha ya hilo nimesumbuka sana maana ninaishi kijijini na huwa naenda mjini kwenye internet cafe kuapply.
Kwa mnaojua sheria je ntazidai vipi? au niende ile tume ya ushindani sijui ambayo hushughulikia malalamiko ya wateja ili wanilipe na fidia.

Nataka ushauri wenu ili nitunze evidences ambazo zingine bado zinapatikana kama za admision closed maana ni kinyume na TCU.
 
Hizi laana nyingine watu wanajitafutia..MTU unadiliki kula pesa ya mlala hoi kama mim namna hii izii tamaa izii...roho ya ukatilii inaanzaga ivii ivii kufanyiana unyamaa
.
 
Pole mkuu system yao haifunguki ukishafanya malipo

Mi binafsi nimeomba second round ikanisumbua hivyohivyo nikawatafuta na wakanitumie form kwenye email
Nimeijaza na nikawarudishia.....
 
Then udahili kwa vyuo vyote ni 10000, kwanini ukalipa 30000?
 
Then udahili kwa vyuo vyote ni 10000, kwanini ukalipa 30000?
Siyo vyote, vya serikali tu ndiyo 10, vingine vina rate yao.30
Pole mleta mada, utashanga pamoja na hela yako kuliwa pia ukiambiwa nafasi zimejaa.
Hili ni tatizo LA TCU kutoku-cordinate kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.
 
universty application "source of income""acha waisome namba eeeee tuliamua wenyewe ......
 
Nimelipia application fees st joh lakini nimeshindwa kufanya application kwa hiyo 10k imeenda bure hii system Tcu na rais wamefail gharama zimeongezeka alaf na usumbufu zimeongezeka
 
Inabidi mkuu uwaendee tu TCU ukawashitaki huko, wanafahamu nini watafanya kwa iko chuo maana wao ndio mabosi.
 
Shule utaiweza kweli!!!!!!
Nashikuru kwa reply yako, hiyo ilikuwa typing error na hasira tu niko vizuri maana nina 1 distinction, one ya 7 na nimepata MD UDOM Namshukuru mungu. Ila sometimes kuwa positive sio kila mtu ankuja kucheza humu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…