Scandinavia wanarudi kwa kishindo

falcon mombasa

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2015
Posts
9,225
Reaction score
9,352
Wakuu mambo vipi,

Hongereni kwa mchaka mchaka wa hapa na pale.

Tuwape pongezi wadau wote wa Scandinavia express baada ya kimya cha miaka mingi sasa wanarudi tena kwa kishindo licha ya kuwa wengine wameamua kutupilia mbali biashara ya usafirishaji lakini scandinavia express wamedhihirisha ukomavu kwa kurudi tena na mabus aina ya scania mabus tayari yamefika salama salmin Dar es Salaam tayari kwa kuanza kazi muda wowote kuanzia sasa.

Je una lipi la kusema?
 
Warudi kwa amani na upendo ingawa vyuma vimekaza
 
Wasifikiri ni enzi zile walikua Wao peke yao Ndio wana Mabus ya Luxury waambie siku hizi mambo yamebadilika sana.
 
Mnapenda kusikia tukisema lakini kuna wengine tukisema na kuwataja majina yao ya sifa inakuwa noma! Diktekta ni shiiiida.

Kwa hili tunasema hiviiiii
TUTAMPA USHIRIKIANO MUWEKEZAJI.

Asituwekee mavideo ya kina lufufu na mabongomuvi, atupie documentaries mwanzo mwisho.
 
Waache speed na pupa za barabarani
 
Mkuu zile Tahmeed vipi nazo mpaka leo hatuzioni barabarani
 
Hizo ndizosa habari!Siyo zile huwa unatuletea eti kikampuni fulani kinatisha kwa basi za kichina!

Scania ndiyo basi bwana!
 
wewe unapenda documentary lakin lazima ukubali wenzio hawataki hata kuzisikia hizo documentary.
 
Acha kudanganya watu mkuu scand yupo zake kwenye malori na ndie mhusika mkuu wa Benbros motors ltd
 
iyo kampuni sijawahi panda gari zake mpaka wanafilisika
mwache aje apambane na new force ambae yupo kila kona kasoro kusini tu
 
Wanatuletea Scania au nao wananunu mabasi ya bei chee kutoka China?
Hapo watakuwa ni China-navia maana watakuwa hawatumii tena magari kutoka Scandinavia
 
na ninategemea watarudisha ile route yao ya Dar s Salaam hadi Lusaka,na kama kuna uwezekano wa basi kuvuka border ya tunduma /nakonde sio kulaza basi pale,tanzania ni muhimu tukatambua kuwa highways ni tofauti na barabara za manisipaa,kuwa na speed limit ya 50km kwenye freeways ni vitu vya ajabu,ila inapotokea freeway inapita kwenye makazi ya watu kama pale mikumi basi pajengwe speed camera za kuthibiti mwendo,sawa na pale mikumi national park zile tuta toa kabisa ule ni uchafu,badala yake jenga speed na timing camera hizi zinarekodi muda unaotumia kupita kutoka point A to B,unapokowa umezidisha speed na camera zimekurekodi unapomaliza tu ile mbuga utakuta traffic officers wanakusubiri na vithibitisho vyote,na ningependa kuona mwanasheria mmoja anajitolea kwenda mahakamani to test the water uhalali wa hizi tochi,kwangu naziona hazina uhalali wowote,na hazina uwezo wa kukusanya vithibiti vyote vinavyoweza kumtia hatiani mtuhumiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…