GE2025 Samia: Pato la wavuvi limefikia Bilioni 38.400 kutoka bilioni 9.400

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kwa miaka mitano iliyopita, serikali ya awamu ya sita imefanikiwa kuongeza pato la Wavuvi kutoka Shilingi Bilioni tisa na Milioni mia nne hadi kufikia Shilingi Bilioni thelasini na nane na Milioni mia nne na hivyo kukuza ajira na pato la wananchi.

Dkt. Samia amebainisha hayo leo Alhamisi Oktoba 09, 2025 Bunda Mjini Mkoani Mara kwenye Mkutano wake wa kampeni Mkoani humo, akiahidi pia kuendelea kuongeza nguvu kwenye sekta ya uvuvi na kilimo pamoja na ujenzi wa Viwanda vya kuchakata mazao ya kilimo na ufugaji kama ilani ya CCM ya 2025/30 inavyomuelekeza.

Amezungumzia pia utekelezaji wa ujenzi wa skimu za umwagiliaji, utoaji wa mbolea na pembejeo za kilimo katika miaka mitano iliyopita, akisema programu hizo zimewesha kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo na uvuvi na hivyo kukuza pato la mwananchi mmoja mmoja pamoja na uchumi wa Mkoa wa Mara akisema Bunda pia imechangia kukuza utoshelevu wa chakula nchini kwa kufikia asilimia 128.

Dkt. Samia pia amezungumzia mahitaji ya skimu za umwagiliaji kwenye Wilaya ya Bunda pamoja na Mabwawa ya umwagiliaji na vituo vya zana za kilimo, akisema ilani ya Chama Cha Mapinduzi imemuelekeza kutekeleza mambo hayo kote nchini sambamba na ujenzi wa kongani za viwanda vya kuongeza thamani mazao ya kilimo, uvuvi na ufugaji.
Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…