Same Hoi kwa Shida ya Maji

Basil Lema

Member
Joined
Jan 20, 2013
Posts
86
Reaction score
277
Hakika ukiwa nje ya wilaya hii ya Same hutawaza kwamba kuna uwezekano wa kuwepo tatizo la maji la kiasi hiki katika mji wa makao makuu ya Wilaya yenye majimbo mawili makubwa. Kibaya zaidi ikumbukwe kwamba wilaya hii imekuwa ikipata bahati ya kuwa na wabunge wanaoukwaa uwaziri kuanzia enzi za Mwl. Nyerere.


​

Kadhia hii ya maji ni alama mbaya sana kwa wazawa wote wa Same waishio ndani na nje ya Same, ni aibu na alama kubwa ya usaliti wa wawakilishi wao hasa waliopata kuwa mawaziri. Kwa hakika ni lazima zitumike nguvu za ziada kuwaokoa watu hawa wanaokatiza usingizi kila siku kwenda kupanga foleni ya maji katikati ya mji.
 

Attachments

  • adha-maji-same.JPG
    69.8 KB · Views: 129
ndiyo matokeo kuchagua wabunge ambao hawana uwajibikaji kwa wananchi mfano anne kilango huyo mama ni bure kabisa kazi kubwa kupika majungu tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…