Sam Mahela kumwambia Hashim Rungwe anaropoka, ni kumkosea adabu

Kwa niliyemfuatilia Sam Mahela kwa muda mrefu jinsi anavyoendesha kipindi cha dakika 45, saikolojia inanipa picha ya mambo mawili makubwa kumhusu mtangazaji huyu:

1. Kuna upande huwa anaegemea kila anapohoji mtu mwenye itikadi au mtazamo tofauti na wake au anayetoa majibu tofauti na aliyonayo yeye.

2. Anafanya kazi zake katika kipindi hicho mindset yake ikiwa imelenga katika kujijenga aonekane kwa mamlaka fulani za uteuzi wala si kwa mwajiri wake. Yuko tayari aharibu kwa mwajiri wake lakini amfurahishe kiongozi wa kisiasa anayemtazama.

Mwanasiasa anayeenda kufanya kipindi na Sam Mahela inambidi awe anajitafakari kama wasifu wake unakaribiana naye kiitikadi na kimtazamo.
 
Mkapa aliwaita WAPUMBAVU NA MALOFA mpaka leo hii kimya kwani kuropoka ni tusi na Rungwe alizungumzia ujenzi wa magorofa ya huko Buguruni tena kwa msisitizo anasema nimepita pale jana tu sijaona kitu chochote labda kama wanajenga underground ila mimi sijaona chochote pale Sam akamuuliza una uhakika? Rungwe ndiyo sijaona chochote pale kwa macho yangu labda nitumie macho yako
.Sasa kama siyo kuropoka nini NB
kuropoka siyo tusi
 
Inategemea ilikuwa katika mazingira gani, musipende kuvifanya vitu kuwa
vigumu.
Kwa mwandishi wa habari kufanya hivyo kwenye mahojiano ni unethical and unprofessional. Amedhalilisha fani na chombo anachotumikia, nani ambaye kesho atataka kuhojiwa kwenye kipindi chake? Ajifunze kwa Albert Chilala wa Channel Ten, kipindi chake ni mubashara lkn haruhusu hisia binafsi kumtawala.


Vv
 
Mwandishi lazima ararajie majibu na asiyotazamia kwenye mahojiano lkn lazima awe reserved na kujua kuwa umma unamtazama, lazima ajitahidi kutunza heshima ya kipindi. Kumbuka, kituo hakiwezi kuadhibiwa kwa kosa la interviewee lkn kinaweza kupata adhabu kwa kosa la interviwer/host.

Vv
 
Aombe radhi ama sivyo achukuliwe hatua na vyombo husika. ili iwe fundisho kwa wengine wajue matangazo mubashara yana kanuni zake ngumi zinge pigwa hapo mjengoni ikawa aibu kwa super bland
 

Kwa hiyo Mkuu unatwambia ile kampeni ya kuua vyama vya upinzani imefanikiwa?, and you are sober and proud of this?? kweli dunia hii maajabu hayataisha.
 
Sam Mahela yaani.sijui nae anaendaga na viroba, alisema Rais Magufuli anaangaliaga kipindi so anataka kumfurahisha rais wake amteue kama alivyomteua Emmanuel Buhohela. Njaa ya madaraka ni mbaya sana
 
Anafikiri atapata ulaji kama wa gg kwa kumwambia mh. Hashim
 
Kabisa uko sahihi, Sam ameanza kufanya kazi zake kwa kutafuta umaarufu flani kwa ili aonekane na wakubwa.. nilikuwa namkubali sana huyu bwana mdogo ila kwa sasa duuuuh amekuwa mnafiki mkubwa sana!
 
Aisee.... Unaweza kuona kwamba lile jina walilopewa watu flani la manyumbu kuwa ni halali yao!

Tundu Lisu na wabunhe wengine wa chadema wanatukana zaidi ya hilo lakini haeajawahi kukemea!
 
Ulushawahi kutoa wazo kama hilo kwamba chadema wamfukuze Lisu kwa kumuita rais anaropoka?
 
Umenena vyema sana mkuu
 
Nazani mindset yako na ya Sam Mahela sawa sawa
 
Angalia tofauti ya umri....within a year mtu anaweza kuwa bilionea
so what do you want to say? kwamba samu anaweza kumfkia kwa mwaka mmoja?, Wapo mawaziri hawamfikii Spunda kiuchumi, huyo Mzee anafanya siasa kwa ajili ya mambo mawiki, ajifurahisha au tuseme anapenda siasa,pili ; anatafuta popularity inayomsaidia kwenye biashara zake . Hata akiingia tra anaweza aspange foleni . Yeye samu huenda anaamini jinsi ya kutusua kwenye maisha ni kwa kupitia kuteuliwa tu.
 
anafwta style ya bashite kumchapa kibao mzee wa watu..i gues alie mwona bashite atamwona nayy ...maana ndo sifa zinazoitajika,kutokuheshima wazee
 
Na mashati yake ya satini na mipiko kichwani hana adabu sam mpuuzi rungwe ni kama baba yake mzazi
 
Rungwe kwa lugha yetu ya kijita ni N.Y.E.G......
Mafia pia kwa lugha yetu hiyo ni M.A.P.U.M.B......
enewei, kama Sam kamwambia hivyo huyo bwana atakuwa amemkosea maana hata ki umri ni mkubwa kwake, ila sasa hatuna clip ya kujua alitamka hivyo katika mazingira yapi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…