Salio la Desi liko wapi?

Tuko

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2010
Posts
11,180
Reaction score
7,356
Nakumbuka serikali ilikomba zaidi ya bilioni moja iliyokuwa imekusanywa katika akaunti ya wale waliokuwa na DESI. Zilienda wapi?
 
Wewe ndio ulikuwa kinara wa huo utapeli? Si bure naona dili limegonga mwamba. Punda wa nyuma kapigwa wewe wa mbele unalia nini?
 
Nakumbuka serikali ilikomba zaidi ya bilioni moja iliyokuwa imekusanywa katika akaunti ya wale waliokuwa na DESI. Zilienda wapi?

Umekumbusha moja kati ya snema zilizotikisa chi muda wake.
Ndivyo tulivyo TZ tunaishi kwa sinema sasa si kuna hii ya watangaza nia!
 
Mimi nilisikia redioni wiki 2 zilizopita kuwa fedha hizo ziko benki kuu wanafanya uchambuzi wa nani alichanga kiasi gani ili hatimaye wanachama wa deci walipwe fedha zao. Lakini ninachojiuliza huo uchambuzi unachukua miaka mingapi? Hii habari ya mwizi kukamata mwizi inatatanisha sana.
 
zilisaidia walokumbwa na mabomu mbagala mbona
 
Hii habari ya DESI imesahaulika hata wahanga nao sijui hawakujua wafuatilie wapi?

Najua salio lilikuwepo ingekuwa vyema kujua hatima ya salio hilo kama ni kurudisha kwa wale waliopoelewa au zinapelekwa wapi kwa manufaa ya wengi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…