Mzee ms inaonekana viongozi wengi wa znz ya nyuma ya miaka 1970 walikuwa na uhusiano wa hali ya juu na serikali ya cuba?
Nakama ndio hivyo nini kimeondoa urafiki huo mkubwa uliokuwepo baina ya nchi hizi mbili znz na cuba?
Sahimtz,
Si rahisi kulijibu swali lako kwa sentensi mbili tatu kiasi cha mtu
kuelewa ilikuwaje Zanzibar ikakumbwa na siasa za mrengo wa
kushoto.
Jana
Salim Msoma mmoja wa vijana waliokuwa na hamasa hizi
kaniandikia kunieleza kwa muhtasari hali ya siasa ya wakati ule.
Ingia hapa:
Mohamed Said: SALIM MSOMA AELEZA KICHWA CHA HABARI: BADAWI QULATEIN ALIANZA KAMA ''COMRADE'' AKAMALIZA KAMA SUFI
Mohamed Said: SALIM MSOMA ANAELEZA SAFARI YA CHE GUEVARA TANZANIA 1965
Kitu kilichokuja kufifilisha uhusiano huu ni muungano wa Zanzibar
na Tanganyika mwaka wa 1964.
Baada ya mapinduzi ilionekana waliokuwa na uoni wa kuendesha
serikali walikuwa ''vijana wa
Abdulrahman Babu'' na
Babu yeye
alikuwa na uhusiano mkubwa sana na China na Cuba.
Karume alikuwa na hofu ya wasomi na kwa ajili hii aliona salama
yake itapatikana chini ya mbawa za
Nyerere.
Nyerere aliitaka Zanzibar kwa sababu ambazo hazikuoana na azma
waliyokuwanayo wafuasi wa Umma Party (UP) ingawa kwa wakati
ule UP ilikuwa ishafutwa na wanachama wake kujiunga na ASP.
Ule uoga wa
Karume wa wasomi ukampelekea yeye kuwahamisha
wanamapinduzi wengi vijana wa mrengo wa kushoto kama
Babu,
Hanga na
Salim Rashid na wengineo kuja Bara.
Hii ilikata ule uhusiano uliokuwapo kati ya vijana hawa na Cuba kwa
kuwa hawakuwa tena na uwanja wa kufanya siasa mbele ya uso wa
Nyerere.
Ingia hapo chini kupata jibu la swali lako kwa kirefu ingawa katika
suala la mapinduzi na ushiriki wa makomredi hii inahitaji maelezo
kwani makomredi hawakushiriki katika mapinduzi kama inavyoeleza:
Abdulrahman Babu: Tanuru La Mapinduzi Zanzibar Na Muungano Lisilokumbukwa VIII – Raia Mwema
Mohamed Said: MASAHIHISHO: SALIM RASHID NA MAPINDUZI YA ZANZIBAR
Mwandishi akifanya mahojiano na Salim Rashid Katibu wa Kwanza wa Baraza la Mapinduzi 1964
TV Imaan Kipindi: Walioacha Alama Katika Historia
Nimekuwekea rejea kadhaa.
Si rahisi kujibu swali kama hili lako inahitaji muda na rejea kadhaa.
Lakini ikiwa unataka kuijua historia hii soma kitabu cha Dr. Harith Ghassany,
Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru na soma kitabu cha Ali Muhsin, ''Conflicts and
Harmony in Zanzibar.''
Kuna mengi yatakayo kustaajabisha kabisa.