Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,242
- 34,917
KAULI ya mkuu wa jeshi la polisi nchini, Simon Sirro, kuwa mwa ndishi wa habari, Silas Mbise, aliyepigwa na askari polisi kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam, alishambuliwa kwa kuwa aliingia kwenye eneo ambalo halifuhusiwi, haikubariki na imelenga kutetea uhalifu nchini.
Hii ni kwa sababu, ndani ya uwanja wa taifa hakuna mahali kokote ambako kumepigwa marufuku waandishi wa habari kufika.
Aidha, mwandishi aliyepigwa alikuwa yuko kazini- kama ambavyo polisi walikuwa wakifanya kazi zao- kitendo cha kumshambulia; na au kumzuia kufanya kazi zake, ni uvunjifu wa katiba.
Hivyo basi, hatua ya Sirro kutetea kitendo cha askari wake kupiga mwandishi, kinapaswa kujibiwa mara moja na waandishi na wahariri kwa kuchukua hatua ya kutangaza, kuchapisha, kusambaza na kupiga picha, habari zote zinazomhusu Sirro na jeshi lake kwa ujumla.
Kwani hiyo ndio silaha pekee ya waandishi ambayo tumekuwa tukiitumia kwa miaka nenda rudi.[/QUOTE
amekurupuka vipi? Polisi walimpiga Mwandishi alafu wanaochunguza tukio ni hao hao Polisi unategemea kupata matokeo ya ukweli? Lazima watamsingizia chochote huyo Mwandishi ili kuharalisha Uonevu wao.kwa mfano wakichukua hatua hizo ndo suluhu ambayo itafanya jeshi la polisi kurudi katika misingi yake? kuna mda kubenea anakurupuka sana.
mchunguzi wa Tukio la kupigwa Mwandishi ni Polisi na huyo huyo Polisi ndiyo mtuhumiwa unategemea nini?Walishindwa kijisimamia kwa kitendo cha kuvamiwa clous tv
Hapo hawawezi hata kwa saa 24
...wakichukua hatua hizo ndo suluhu ambayo itafanya jeshi la polisi kurudi katika misingi yake?
Wewe ambae haujakurupuka kutoa coment ebu tuambie waandishi wanatakiwa kufanya nini badala yake?kwa mfano wakichukua hatua hizo ndo suluhu ambayo itafanya jeshi la polisi kurudi katika misingi yake? kuna mda kubenea anakurupuka sana.
acha hizo kule Dodoma Kamanda kutwa yupo na vyombo vya habari hata makamanda wengi wanapenda vyombo vya habari ili waonekane wapande vyeo.Kubenea anamaanisha waandishi walitenge jeshi la polisi? Jeshi la polisi halihitaji kutangazwa, matokeo ya kazi zake ni matangazo tosha kwa wananchi. Kubenea atakua anashida sehemu kichwani kwake.