Saa

Viol

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Posts
25,419
Reaction score
18,368
Mama moja alipofariki alijikuta amefika mbinguni,malaika akamchukua na kumtembeza ili kumwonyeshea maajabu ya huko mbinguni,akamwonyeshea saa mbalimbali za mishale zikizunguka haraka haraka na pole pole,hizo saa zilikuwa zinawakilisha dhambi na matendo ya watu,malaika akamwambia saa zinazoenda pole pole ni wale ambao walikuwa hawana dhambi nyingi,na saa zinazoenda haraka haraka ni wale ambao wana dhambi nyingi.Malaika akamwonyeshea saa za mtume Paulo,Peter,Musa na wengine wengi,saa za hao mitume ilikuwa inazunguka taratibu sana,akaonyeshewa tena Saa za kina Hitler na Idi Amin,yaani zinaenda kwa spidi ya haraka sana.
Yule mama akamsihi malaika ili aone saa ya mmewe,malaika akamwambia saa ya mme wako ndo inatumika kama feni humu ndani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…