Dawa ya hao wanaotaka rushwa ya ngono ni kuwawekea mtego ili wakamatwe kwani hii tabia inarudisha nyuma maendeleo ya watoto zetu Pia kueneza maradhi vyuoni hasa ukimwi.
Wanajipeleka wenyewe, yaani katika kundi la wanafunzi zaidi ya mia mbili huyo mhadhiri anaanzaje kukujua bila kujipeleka?
Halafu wengi wao hawajiamini, ni vilaza, hivi mtu course work inasoma 31 huyo mhadhiri anaanzaje kukutishia kukufelisha?
Kama wanapeana wapeane kiroho safi wasisingizie rushwa.
Ngono na uzinzi umetawala kuanzia watoto hadi wazee,matajiri hadi maskini ,wanasiasa na wanachama wao,maamuma na wasomi .
Kila sekta ngono imetamalaki,hakuna tena anayeona kama hilo ni kosa.Na imekua ni fasheni kwa wanawake hasa akiombwa ngono na mtu mwenye mapesa au chei kikubwa kwake ni ufahari kwani ndugu zake ,wazazi na marafiki watatambulishwa na kujulishwa habari za uzinzi huo na itaonekana kama ni bahati nzuri kwa huyo mwanamke ,mara nyingine hata kama ana mume basi na mwanaume anaweza akajua na akajikausha kwani utajiri umeingia nyumbani.
Hapo nani wa kumvisha paka kengele.
Ukiwatega na kuwachukulia hatua basi wahadhiri wenzake watawafelisha wanafunzi kwa maksudi mpaka wakome. Assignment zote Total marks 12%;End exiam 22% -Total 34%-(Failed).
Kwani wahadhiri wa vyuo vikuu wanakozi za kufundishwa maadili ya kazi?
Au mtu akishaonekana jembe kwenye masomo yake basi akiomba nafasi ya uhadhiri anapewa?
Matokeo yake yatabaki kama tabia ya mtu binafsi.
Habari Wana Jamii Forums,..
Kuna hili suala la rushwa ya ngono ambalo limekithiri vyuoni.
Baadhi ya wahadhiri wa vyuo vikuu wanalazimisha mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi wao, inapotokea mwanafunzi kumkatalia mhadhiri basi anakuwa matatani kwani wahadhiri hao huwatamkia waziwazi wanafunzi hao kwamba watawafelisha katika mitihani yao.
Ikumbukwe kuna wanafunzi wanafaulu kwa jitihada zao binafsi na kuna wale wanaofaulu kwa kutoa rushwa ya ngono.
Hebu tutafakari basi, ni nini kifanyike maana suala hili lina changamoto kubwa.
Je mwanafunzi akatae kutoa rushwa ya ngono afeli au atoe rushwa ya ngono apate kufaulishwa!!
Pia nini kifanyike kwa baadhi ya wahadhiri wenye tabia hii chafu ya kutaka rushwa ya ngono ambayo inawaathiri wanafunzi katika taaluma!!
Nawasilisha,...