Naunga Mkono hoja ya Mkuu Capo Delgado!
Uongozi wa Simba, hasa Try Again na Magungu! Inawezekana sio watu wa Mpira kama inavyosemekana!
Haiwezekani timu msimu wa tatu huu wameshindwa kutatua tatizo la kiungo mkabaji wa uhakika!
Kwa Sasa tunaweza sema tuna Ngoma, lakini asipokuwepo tu ,tunarudi kwa kina Mzamiru na Kanuote ambao wana kasoro nyingi kiuchezaji!
Viongozi wameenda kuongeza tatizo lingine kwenye beki wa kati, beki wa kushoto na golikipa!
Asipokuwepo Inonga au Che- eti sub ni Kennedy!
Kwa Shabalala- sijui sub ni nani!
Umefanyika Uzembe wa kumuacha Kakolanya, Huku wakijua Aishi anaumwa!
Mwisho! Binafsi sikuona haja ya kumtoa kocha Mgunda!
Huyu Robetinho- naomba boli halitembei kabisa!
Butua butua na anao anao nyingi sana!
Ingawa ligi ndio inaanza- ila inatia mashaka kidogo!
Mwisho! - au ni kweli yule Marehemu Hans popu- ndio alikuwa bingwa wa ku- scout