Ripoti ya 2018 ya CAG - Mkaguzi na Mdhibiti mkuu kuhusu Daissy General Traders

KING MIDAS

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
10,569
Reaction score
21,075


‼️TUJIKUMBUSHE‼️
Ripoti ya 2018 ya CAG - Mkaguzi na Mdhibiti mkuu kuhusu Daissy General Traders ilisema:
“Nilifanya Ukaguzi huu kufutia maombi kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKURURU), na kwa mujibu wa Kifungu 29 na 36 ya Sheria ya Ukaguzi wa Umma Na. 11 ya 2008. Kazi hii ilifanyika kwa kuongozwa na hadidu za rejea zilizoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya
Ukaguzi. Lengo la Ukaguzi huu lilikuwa kubaini kama Manunuzi ya sare za Jeshi la Polisi yalitekelezwa kwa kufuata sheria na kanuni za Manunuzi ya Umma, na kuthibitisha kama malipo aliyolipwa Mzabuni Daissy General Traders ni halali na yalihusu Sare alizoleta,kupokelewa na kuhifadhiwa na Boharia Mkuu wa Jeshi la Polisi. Katika Ukaguzi huu, yafuatayo ndiyo mambo ya msingi yaliyoibuka:
👉🏽12.2.4.1 Maoni ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Hayakuzingatiwa
👉🏽 12.2.4.2 Malipo ya Sare za Polisi ambazo Hazikuletwa Kwa Boharia Mkuu wa Jeshi la Polisi Sh.16,660,000,000
Hapa anaeleza CAG:
👉🏽 Kukosekana kwa nyaraka za kuthibitisha uletaji wa mzigo.
Niliomba Hati ya kupokelea Shehena ya Mzigo Bandarini (Bill of Lading), Hati ya Madai kutoka kwa Mtengenezaji (Commercial Invoice), Hati ya Mzigo ulipotoka (Certificate of Origin), orodha
za mali zilizopo kwenye meli (Packing List) na cheti cha ukaguzi wa bidhaa (Inspection Certificate) kutoka kwa Mzabuni Daissy General Traders kwa ajili ya kujiridhisha kama bidhaa husika
zililetwa nchini. Hata hivyo, Mzabuni alishindwa kuwasilisha nyaraka hizo.

Angela Kizigha shostiake @SuluhuSamia leo amepewa tenda za jeshi
#TutaelewanaTu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…