Makoye Matale
JF-Expert Member
- May 2, 2011
- 6,490
- 2,104
Simba wamechoka wameamua kujifua mchangani.
Simba SC ya Dar es Salaam leo imelazimisha sare ya ugenini baada ya kufungana bao 1 kwa 1 na Rhino Rangers FC ya Tabora. Mchezo huo ulipigwa katika dimba la Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora. Simba ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 35 kupitia Singano aliyepiga penati. Dakika ya 43 Rhino walisawazisha bao hilo. Kocha wa Simba JULIO amelalamikia maamuzi ya mwamuzi mmoja ambaye hakumtaja (Source: Spoti Leo, Radio One Stereo).
Mchangani unamaanisha nini? hiyo timu Rhino Rangers imepanda daraja msimu ujao inacheza Ligi Kuu ya Vodacom.
Wamejitahidi! timu za mikoani kama kawaida wanakamia mno!
Simba SC ya Dar es Salaam leo imelazimisha sare ya ugenini baada ya kufungana bao 1 kwa 1 na Rhino Rangers FC ya Tabora. Mchezo huo ulipigwa katika dimba la Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora. Simba ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 35 kupitia Singano aliyepiga penati. Dakika ya 43 Rhino walisawazisha bao hilo. Kocha wa Simba JULIO amelalamikia maamuzi ya mwamuzi mmoja ambaye hakumtaja (Source: Spoti Leo, Radio One Stereo).
Sasa hapa aliyelazimisha sare ni rhino au simba? unajua maana ya kulazimisha sare?
ndo wakurupukaji hao tushawazoea..
Nilitegemea post kama hii! Rhino ni timu mwenyeji ilikuwa na nafasi kubwa ya kushinda kwa vile iko nyumbani (Home Ground Advantage), kitendo cha Simba kupata sare ugenini ni 'Kulazimisha sare', ingekuwa ni mechi ya mtoano kwa sare hii hii, Simba angesonga mbele kwa mabao 2-1 yaani 'Faida ya Bao la Ugenini, (FBU)' hii ndiyo maana ya kulazimisha sare! Siyo eti kwa sababu Rhino kasawazisha, ndiye kalazimisha sare! Nadhani umeelewa.
Thanks for the new term.Kwa hiyo Simba walizidiwa wakaona ni bora walazimishe sare kuliko kufungwa? asante kwa kunipa maana nyingine ya neno "Kulazimisha sare"
Hajui anachokisema,ni vema ulivyompa darasa!Mchangani unamaanisha nini? hiyo timu Rhino Rangers imepanda daraja msimu ujao inacheza Ligi Kuu ya Vodacom.