Nafikiri anatania kutokana na sababu alizotoa; mojawapo ni kusimamia kilimo ambacho wananchi wa Ulanga Magharibi watalima mara moja tu na kuvuna kila mwaka bila kulima tena bila kusema ni mazao gani hayo. Sasa sijui anajua mazao yanayostawi ulanga. Ukiangalia kwenye Socio - Economic profile ya Mkoa wa Morogoro ya mwaka 2002 pp. 49 na 54 mazao yanayolimwa sana Ulanga ni pamba, sunflower, simsim, karanga, 'pigeon peas', mahindi, mpunga, mhogo, mtama, ndizi, viazi vitamu, na maharage. Sasa kati ya haya ina maana atashughulikia yale ya muda mrefu tu. Au atayabadilisha yale ya msimu mmoja kwa mwaka ambayo ni mengi kuwa ya muda mrefu! Atayabadilishaje, hakusema. Anandandia Kilimo Kwanza bila kuelewa!
Pia sielewi alivyosema kuwa atatumia uzowefu wake wa kufanya kazi chakula na lishe, usalama wa raia, NSSF na ITV katika kuimarisha kilimo. Huyu akiwa mbunge ni sawa na kubalisha spea kwenye engine ya gari kwa kuweka used, tena spea yenyewe ni sensor muhimu sana!!