Ndio laana ya UZINZI na maisha yasiyompendeza Mungu.
Mungu huwaumbua wabaya kwa matendo yao na huo ndio mtihani aliojitakia shoga yako, baba yake na mama yake shoga yako.
1. Baba anamkataa mtoto wake na kuishi maisha yote bila kukumbuka kama ana binti, kosa la kwanza. Kosa lake la pili, ni kuacha ndoa yake na kurukaruka nje. Amefikia hata kuzaa tena. Haya ni maisha ya wanyama
2. Mama yake shoga yako naye ni mpumbavu pia. Kauli yake ya kwamba kupata mimba ni jambo jema inadhihirisha si mzima kichwani. Mimba bila ndoa ni majaribu sio jambo jema. Na angeambiwa kabla angebisha, lkn sasa wote twaona kuwa ni jaribu. Kama binti angempeleka huyo mwanaume kabla ya kuingia naye masuala ya mwili basi ilikuwepo nafasi ya kuzuia uharibifu huo.
3. Shoga yako ndie mpumbavu hasa. Hivi msichana anayefanya urafiki na mume wa mtu ilhali akijua ni mume wa mtu huwa na akili ipi? Kwa mimi halinishangazi sana kwani uharibifu wa dunia hii ulianzia kwa mwanamke, lkn na wengine mnajiuliza hili?
Binadamu tusiishi kama wanyama. Sasa kwa haya tujifunze kwa hili hususan wewe ambaye naamini katika hatua za mwanzo uliona kuwa rafiki yako amepata bahati, na si ajabu hata ulimuonea wivu.