Mimi sikubaliani na wewe, kwa sababu nikishajua ninachotaka nikutafute wewe ili iweje? Mm nnachofahamu ni kwamba kuna baadhi ya watu hawana idea kabisa kuhusu kuchora raman hata ya nyumba yake, ila unapompa sample ndipo atakapokuambia iko sawa, Punguza au ongeza hiki, sasa ww unataka mm niwe na idea naitoa wapi?
idea ninayoizungumzia hapa ni kama hivi
1. Mimi plot yangu ni 15 x 18 mita.
2. Nataka ramani ya vyumba vitatu simple ndani iwe na jiko stoo isiwemo, dining, sitting, choo cha jumla.
3. kuwe na baraza kubwa mbele na ndogo upande wa jikoni
4. iwe na paa za kona kona ndio mi napenda
5. mahusiano ya vyumba iwe hivi, master iwe mbali na vile vyumba vingine viwili
6. ukiingia tu mlango mkuu kulia kwako iwepo dining lakini isiwe room separate, pia choo cha jumla kiwe na bafu na sehemu ya kupiga mswaki
7. njee ya nyumba usiweke parking mi sina na sitakuwa na kigari ila weka kiveranda fulani hiv kwa mbele cha kupaki pikipik na baiskeli yangu.
8. usiweke urembo mwingi na madoido sitaki, iwe nyumba ya kishikaji tu
9. vile vibaraza visiwa vya kumimina cement ni gharama chonga vya bati kiana
hapo sasa mtalaam atakupa kitu roho imetaka