Kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu, Ramadhan Njala Jumanne ameweka wazi nia ya kugombea ubunge katika Jimbo la Geita vijijini kupitia chama cha ACT Wazalendo.
Bw. Ramadhan ameweka wazi baadhi yaa vipaumbele vyake ambapo amesema lengo lake kubwa ni kuhakikisha anaunganisha wakazi wa Geita vijijini na kutetea maslahi mapana kwa kila mwananchi.
Naye Katibu wa Jimbo la Geita Vijijni Bw. Francis Masayi amesema chama kimelazimika kumteua Bw. Ramadhan kupeperusha bendera ya chama cha ACT Wazalendo katika eneo hilo.