Rais wa FIFA aipongeza Yanga FC kwa kubeba kombe la VPL

Faru fausta

JF-Expert Member
Apr 29, 2017
218
143
a6a905d6ce20221ac900f5fa749f09e5.jpg
[https://2]

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kimataifa (FIFA), Gianni Infantino, Mei 24, mwaka huu alituma ujumbe Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuipongeza Young Africans ya Dar es Salaam kwa kutwaa ubingwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2016/17.

Young Africans imetwaa Kombe hilo ikiwa ni mara tatu mfululizo na katika salamu za pongezi, Rais Gianni Infantino amesema ubingwa huo wa Young Africans ni kielelezo cha ushirikiano baina ya wachezaji, kocha, utawala, matabibu pamoja na mashabiki.

Katika pongezi zake Rais Infantino ameishukuru Young Africans na shirikisho la mpira wa miguu la nchi kwa kusadia kupeleka ujumbe chanya kwa jamii kuhusiana na mpira wa miguu.
 
Lakini viongozi wetu ni TATIZO. Yaani Yanga na Simba zinavyotumia fedha nyingi kwenye wachezaji wa nje ni AIBU. Bora Yanga wanaibiwa na kombe wanabeba kuliko hao wenzao
 
Kawakomoa
 
Lakini viongozi wetu ni TATIZO. Yaani Yanga na Simba zinavyotumia fedha nyingi kwenye wachezaji wa nje ni AIBU. Bora Yanga wanaibiwa na kombe wanabeba kuliko hao wenzao
Hili Suala linahitaji Mjadala mpana sana kutoka kwa wadau wa soka.

Sijui tatizo ni mawakala au ndo ile 10% kuna wachezaji wanakuja huku kucheza hata wale wa ndondo cup wana viwango zaidi yao.

Bravo sana kwa Kamusoko anajitambua amepambana mpaka ameitwa Timu ya Taifa.

Kuna Timu ilikua na wachezaji wengi sana wa kigeni ila wameshindwa kusaidia kabisa.

Bravo kwa Meck Mexime Bonge la kocha Kagera Sugar pale hakuna wageni ila kafanya mambo makubwa.

Mwaka jana walitaka kushuka Wamshukuru Adolf Rishard kawaokoa ila msimu huu no 3 ndo tunaweza kuyaita maendeleo sasa haya.

Bado zinatakiwa sheria Nzuri kuhusu wachezaji wa kigeni toka Tff.
 
Hakuna guarantee kuwa kila mchezaji wa nje anayesajiliwa lazima awike. Kuna wengine wanatoka kwao wakiwa wanachezea timu zao za Taifa na viwango vya juu sana, lkn mara wafikapo hapa wanageuka vichekesho, halafu wakirudi tena kwao wanakuwa tishio tena. Kwenye mpira kuna mengi ila inaonekana mazingira yetu sio rafiki kwa wanasoka wa kulipwa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom