Rais wa DARUSO alikoroga UDSM

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), wamemtuhumu Rais wa serikali yao, kwa kukiuka katiba na kutumia nafasi yake kufanya mambo ya hovyo badala ya kutetea maslahi ya wasomi hao ikiwamo kuwasemea waliokosa mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka jana.

Wasomi hao wamesema Rais huyo Jilili Jeremiah anatumia nafasi yake kuwalazimisha wanafunzi wenzake wakubaliane na mawazo yake binafsi ya kumpongeza John Magufuli kwa kukataa kuongeza muhula wa uongozi kutoka miaka mitano hadi saba.

Wamesema masuala hayo anayotaka Rais wa DARUSO hayawasaidia wanafunzi kutatua kero zao ikiwamo baadhi yao kukosa mikopo kwa ajili kugharamia masomo yao.

Kutokana na hatua hiyo ya Jeremiah, Bunge la wanafunzi limepanga kuitisha kikao cha dharura ili kukuanya saini za wanafunzi kwa lengo la kumvua madaraka haraka kwa kuwa ameanza kufanya mambo ya hovyo ambayo hayalengi kuwatetea wanafunzi.

Makamu wa Rais wa DARUSO, Anastazia Antony na Spika wa Bunge la wanafunzi, Deogratias Mahinyila wamempinga kiongozi huyo huku wakisema suala la kumpongeza Rais Magufuli lingetakiwa kuwa la kwake binafsi na siyo la wanafunzi wote.

Wamesema kiongozi huyo ni kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), hivyo angetoa pongezi binafsi badala ya kuingiza wanafunzi wote huku akijua suala hilo haliwasaidi kitu.

Katika hatua inayoonekana kuongeza mgogoro zaidi, Rais wa DARUSO, ametangaza kuwavua nyadhifa za uongozi Mawaziri wawili wa serikali ya wanafunzi ambao pia waliipinga tamko lake la kumpomgeza rais Magufuli.

Rais huyo ametengua uwaziri wa Matata Juma aliyekuwa waziri wa Mikopo kwenye serikali hiyo pamoja na naibu wake Marobo Stanilaus na badala yake amemteua Gadson George kuziba nafasi ya Matata.

Amesema kuwa viongozi wa DARUSO hawakuunga mkono tamko hilo kwa sababu halikuwa zao za mjadala wa Serikali hiyo na kwamba ni matakwa binafsi ya kiongozi huyo.

“Kama mjadala wa muda wa urais katika taifa letu haukuwa mwema kama alivyodai Rais wa DARUSO, kwa nini hakuupinga hadharani huko nyuma, lakini amesubiri kupongeza msimamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu ya jambo hilo”

Matata ambaye amevuliwa madaraka ameeleza kuwa sababu zilizosababisha kuondolewa kwenye serikali hiyo ni hatua yake ya kupinga waziwazi tamko la Rais wa DARUSO kutokana kuwa ni tamko lilojaa hisia binafsi.

Amesema kuwa tamko lilitolewa na Rais huyo siyo la kisomi na kwamba wakati wote amekuwa akitumia vibaya nembo ya DARUSO kwa maslahi binafsi.

Amesema kuwa wanafunzi wa UDSM wana shida ya mikopo lakini Rais hakuwahi kuyapa kipaumbele badala yake amekuwa mtu wa kupongeza.
 
Hao wanaompinga tutawaondoa chuo mara moja warudi kijijini kulima nyanya
 
Shenzy kabisa anataka kutuletea mambo ya baba Jeska hebu aingie darasani huko asituletee laaana nyingine kwa vijana wetu
 
Rais mwenyewe alisema vyuo iwe sehemu ya kusoma sio kufanya siasa sasa wao wanataka kuanza mambo ya kisiasa kwa kumpongeza rais ili iweje? Je ikifika mahali pa kumpinga napo watatoa tamko la pamoja?
 
Wanaoongoza kukusanya sahihi wakijapotea tusitafute mgonjwa shambani.

Expansion joints and settling ilianza vivyo hivyo.

Nitarudi tena.
 
Makada wa ccm wanashindwa kujenga hoja wanalazimisha mambo ona sasa anatengeneza migogoro isiyo ya lazima
 
Siku hizi UD kuna vitoto vinavyojua kuiga mitindo tu basi, watoto wa kiume wamekuwa walaini kwasababu ya kubugia chips ...kama mmechoka kusoma rudini mtaani tule wote ugali, nyinyi hamfaii kwa nchi yetu. Hamjuhi lipi jema na lipi baya
 
MMeiharibu UDSM yetu. Toka lini uongozi wa DARUSO ukawa ni uwanja wa kutoa matamko ya pongezi? Huyo Rais wa Daruso ingekuwa enzi zetu angeshafukuzwa ofisini zamani. Mnaitilia aibu taasisi kubwa kama UDSM kwa maslahi ya kuonwa na viongozi wa serikali. Enzi zetu DARUSO na kiongozi yeyote wa serikali au wa chama tawala ilikuwa ni paka na panya. Rais wa Daruso alipaswa kwanza awe kipanga. Leo Rais wa Daruso ana sup za kutosha na kilaza wa kutupwa ndo anapewa hiyo nafasi. Poor our beloved UDSM! What has gone wrong to the extent that DARUSO 'leaders' are NOT Leaders? Shame on you.
 
Inakuwaje kada wa chama tawala akapata uongozi ndani ya DARUSO? Hapo hakuna DARUSO bali uchuro mtupu! Wenzenu wapo mitaani kwa kukosa mikopo nyie mnapoteza muda kuandika matamko ya pongezi.
 
Vinara wakupinga hizo pongezi msishangae wakaben saanane
 
UDSM ilikua zamani...sio sasa mnagomea mkopo Rais wa UD alikua mtu anajulikan nchi nzima hii...
 
What!!! Mwacheni apongeze ndio zama hizi zinataka Hawa jamaa wanahitaji Kunji za kileo mkileta zile za wakati wetu watawafanyia kitu mbaya.

Bwana Juma anaelewa zaidi akipongezwa Na kutukuzwa, Na Hawa watoto wamesoma mchezo Kama Mzee Lowasa kaliona game tough huyu dogo wadaruso msuli WA kukaza anautoa wapi.
 
Shida ambazo wanakabiliana nazo wanafunzi wakiwa chuoni ni shida ndogo ndogo na zinavumilika. Wajiandae kwa shida nyingi zaidi (dhiki kuu) wakisharejea huku mtaani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…