Rais Samia Mwondoe Kigogo huyu Arusha

nyamadoke75

Member
Joined
Apr 1, 2020
Posts
95
Reaction score
288
Mimi Kama mtumishi wa serikali nimekuwa nikiwaletea mwendelezo wa madudu ya Katibu tawala wetu mkoa wa Arusha, Athumani Kihamia ikiwa ni sehemu ya nne ya kuujulisha umma ubabe wa kiongozi huyo kutumia dhamana ya cheo chake ,kukandamiza watumishi wa hususani wa halmashauri ya jiji la Arusha mara baada ya kufanikisha mpango wao wa kumng'oa aliyekuwa mkurugenzi wa jiji ,John Pima.


Kupitia kaimu mkurugenzi wa jiji ambaye inasemekana hana maamuzi yoyote tangia akaimishwe nafasi hiyo zaidi ya kupokea maelezo ya Kihamia, hivi sasa Kihamia amekuwa akimpa maelekezo ya kusimamisha watumishi waliokuwa karibu na dkt John Pima ,ambapo hadi sasa watumishi wanne wamesimamishwa kazi akiwemo Merry Mwita,Zulfa,Peter na Honest ambao walifanya kazi kwa karibu na Dr.Pima kwa madai kuwa walikuwa Chawa wa Mapato.


Hata hivyo kwa ubabe wake Kihamia amewapa madaraka wasambaa wenzake kuwa wakuu wa shule za jiji bila kuwa na vigezo wala uwezo ,akiwemo Shamda Athumani Mkuu wa shule ya Felix mrema,Ndeenengo Paulo mkuu wa shule ya Kalimaji,Anton Piuse mkuu wa shule ya Ngarenaro,Alawi Athumani mkuu wa shule ya Olmoti,Adam Abraham mkuu wa shule ya Ungaltd na Annasa Mgunya wa ungaltd huyu ndio katibu katawala mwenye maamuzi mezani kwakwe.



Ubabe wa kigogo huyo kumepelekea kuwa na msuguano wa chini chini na Mkuu wa mkoa wa Arusha ,John Mongela kwa kupuuza maaelekezo yake mara kwa mara akijidai anasimamia sheria na sio kufuata matamshi ya mdomo jambo ambalo linazidi kuwaweka njia panda wananchi ambao wamemwomba rais Samia suluhu kumwondoa kigogo huyo haraka anayevuruga viongozi wenzake Arusha kwa maslahi yake binafsi.
 
Unaposema hao walimu hawana sifa na vigezo una manisha hawana degree kwamba Wana diploma?

Nijuavyo Mimi ili uwe mkuu wa shule sifa ni kuanzia mtu mwenye degree na kwa upande wa primary ili uwe mwalimu mkuu ni kuanzia diploma.

Fafanua Hilo tofauti na hapo Basi utakua umepokonywa shule hapo jijini.
 
Huyu Kuhamia ni jipu la muda sana haliivii tu au ndio u...d....I....kazini
 
Jiji la Arusha ni cosmopolitan city, kuna watu kutoka Mikoa yote ya TZ, ila kuna shida ya ndugu zetu wa kichaga waliojimilikisha jiji hili na huwa wanawapinga wenzao ambao sio wa kabila lao au sio kibaraka wao.

Huyu kigogo anapigwa vita sana na walafi wachache waliokuwa wapigaji wakubwa wa miradi ya jiji
 
Ni mdini na Mkabila HAFAI

Taarifa TUNAZO....
 
Acha ushabiki taarifa zake tunazo UKABILA kawafukuza watu wengi hapo kisa U western....ndo maana bro wa Ukerewe anapata KIZINGITI
 
Hayo ni majungu tu huyo kihamia ni kiongozi Bora sana fanyeni kazi acheni uchonganishi
 
Paka mkubwa aliondoka, sasa purukushani za panya kila kona ya nyumba😅
 
Wewe sukuma gang wacha ukichaa wako ebu fanya kazi .

Habari za ubaguzi wa kikabila hautakuwacha salama na baba yenu aliyekuwa anawafundisheni huo ubaguzi hayupo nanyi tena.
 
Sukuma gang lazima mnyooshwe this time around.
 
Kastory kenyewe kamekaa kimbeya Mbeya, kimajungu majunguuu, halafu mnamsumbua rais.Kama wewe ni mzalendo kweli jitaje jina basi Ili uchunguzi uanzie kwako
 
Huyu jamaa hata mimi simkubali hata kidogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…