GE2025 Rais Samia aahidi Kukamilisha Ujenzi wa Tawi la UDSM Kagera

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
505
Reaction score
887
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kusimamia kukamilika kwa ujenzi wa tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mkoani Kagera, ambalo limefikia asilimia 70 ya utekelezaji. Amesema, iwapo ataendelea kuaminiwa kuongoza serikali, atahakikisha chuo hicho kinakamilika na kuanza kutoa huduma ili kuwanufaisha wananchi wa Kanda ya Ziwa kupata elimu ya juu kwa urahisi zaidi.

Dkt. Samia ametoa kauli hiyo Alhamisi, Oktoba 16, 2025, wakati akizungumza na maelfu ya wananchi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika Viwanja vya Kaitaba, Bukoba Mjini, mkoani Kagera.

Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…