Tambua mikataba sio msahafuMkuu haya makampuni ya madini yaliingia humu nchini na yapo kisheria.
Tulitengeneza mikataba sisi wenyewe kupitia bunge letu lenye wabunge wengi wa CCM likapitisha hiyo mikataba with majority votes.
Tusijitoe fahamu hivi sasa kama vile hawa watu wameingia huko kwenye migodi illegally.
Mwenyekiti alikaa akatafakari kwanini Tanzania iendelee kuwa ombaomba wakati tunapigwa kwenye madini.Mwenyekiti akasema, nchi ni tajiri inaweza kujiendesha bila kutegemea mikopo.
Thubutuuuu baadaye kidogo akapokea mikopo ya fasta kutoka WB kisha akamuomba Zuma amjengee reli, reli ambayo alituambia tuna hela yetu inayotosheleza kuijenga yote.
Mleta uzi una maono ya Mwenyekiti, hutaki kua tegemezi lakini unapingana na ukweli kua ili kuacha utegemezi lazima kuwe na mchakato. Mchakato wenyewe siyo wa kushindiliana kodi na kuwaconvert trafiki wawe wakusanya mapato.
Na au kula rambirambi maana majanga hayatokei kila siku.
Bahati mbaya think tank wa chama wamemkera wamemtaja kwenye ripoti, sijui atabuni nini lakini ni dhahiri nyoka wa makengeza msaka pesa wamemuudhi.
Sasa hivi nani atakua anawapa dira?
Bashite?
Kuna uzi unasema hatimaye acacia wakiri hawajasajiliwa una ufafanuzi mzuri tu.Watanzania acheni woga, mbona mnapenda kuwa na fear of unknown?
Kosa kubwa kabisa la Acacia ni kutotambulika kisheria nchini, kosa la pili ni ku-underdeclare ya huo mchanga wa makinikia, unadhani Kwa akili yako, huyo Prof. Mruma na timu yake eti watakuwa wamekosea? weeee!!! thubutu....!
Acacia ni lazima wazungumze hivyo ili kuwapoza shareholders, ndio maana umesikia huyo Chairman wao kaja.
Mkuu Bowie unaipenda nchi yako lakini ujue maarifa namna ya kuingia mikataba tunapungukiwa. Imagine wb akija na sharti la weka masharti mazuri kwa wawekezaji. Being out of world system is the best option.Baada ya ripoti ya kamati ya madini kutolewa ni uhakika makampuni yaliyoathirika na ripoti hii yataanza kutumia mawakala wao wakubwa World Bank na IMF katika kuishindika serikali ya Tanzania ili kuwe na makubaliano ambayo yanaweza kuendelea kuileta hasara nchi hii.
Pamoja na mikopo tunaopewa naona mashirika hayo lakini mikopo yao ni kama chambo katika kukamatia samaki
Hivi karibuni Rais wa World Bank na baadaye makamu wake walifanya ziara hapa Tanzania.
Ni Word BankNadhani unatakiwa kufahamu role ya hizo taasisi kwenye issues kama hizi!!! Kama Acacia hawataridhika na kuamua kutafuta njia za kisheria hususani zile zinazowalinda, basi suala la hizo taasisi halikwepeki na JPM hana choice!!
Sina kumbukumbu vizuri... ni ama World Bank (75%) au IMF (25%), mmoja wao ni mdhamini wa hizi multinational investments. Udhamini unaoweza kuwafanya wao wawalipe hao investors inapotokea mambo kama haya!!!
Itakuwa unaumwa degedege wewe.Tumempata Rais Mzelendo
Kiukweli Huyu ndiye Rais bora na anaye tufaa watanzania
tunahitajika kumuombea Rais wetu