Rais kuingilia taratibu za ibada

Na we we pia kapanue ubongo,
Kufagia ama kusafisha siyo lituljia ni majitoleo,
 
Ona aibu acha uongo,
Katoliki haipo holela hivyo ndo maana hakuna kashfa za wizi wa sadaka,upo utaratibu wa kilituljia wa ukusanyaji sadaka na namna ya kuzipeleka altareni,usidhani unajiendea tu km unavyoenda chooni,altale ilipo kukiwepo Ekaristi tu huwa panapewa utakatifu maalumu sababu tunaamini Kristo mwenyewe huja,ndo maana kuna utaratibu wake wa kufanya lolote pale
 
Nadhani una matatizo kichwani mwako. Dkt Magufuli kalelewa na wakatoliki anafahamu taratibu zote! Wewe utakuwa ni mkatoliki wa vyama vya upinzani, ukome kushobokea vitu visivyokuhusu.
Duh kumbe wakatolik mpo makundi mawili
A-Wanaomshobekea Rais bila ya shaka wanaongozwa na PENGO
B-Wakatoliki wa upinzani hao kiongoz wao bado hamjatuambia
 
Nimemuelewa sana muanzisha uzi. Si jambo baya kujitolea kufanya jema pale inapolazimu. Kwa jinsi nilivyoangalia clip ya juzi na kama muumini mkatoliki nayasema haya:-

1. Tukubaliane tu kuwa mtu yeyote maarufu anapofanya jambo mbele ya hadhara hata kama ni dogo ana uwezo wa kuvuta hisia na "attention" ya watu kutoka katika kile wanachofanya kuelekea kwake kwa maneno mengine (he becomes a centre of attention). Na katika jambo kama la kuabudu ambapo MUNGU ndiye kiini cha kusanyiko inakuwa si vyema sana.

2. Kwenye video niliona watu wa usalama na walinzi wa raisi wakizuia watu kumsogelea rais. Ikumbukwe ile ni Misa na si mikutano ya hadhara hivyo kila mtu katika kutoa sadaka angependa kufanya hivyo katika moyo wa ibada bila kuzongwa. Hilo ni kosa.

3. Na mwisho, kama lililofanyika Mbeya linatokea kila mara Parokia ya Oysterbay basi sina shaka kuwa Mh. Magufuli aone tu kuwa ni busara kuwaacha wasaidizi wa misa ambao kila Jumapili wanachaguliwa kwa kazi hiyo wahudumie watu. Ikumbukwe Magufuli akinyanyuka kanisani na wasaidizi wake wanalazimika kumlinda hivyo kunaharibu utulivu wa kuabudu.

USHAURI WANGU: Mh. Rais aige tu kwa Nyerere ambaye alionekana mnyenyekevu Kanisani hata bila ya kuzunguka na kapu la sadaka. Kuna mambo mengi ambayo si dhambi ila yakifanywa mahali sipo yanaleta "disorder" na hili si lazima mtu awe maarufu. Hata akitokea yeyote yile Kanisani akaanza kujichukulia kapu la sadaka kukusanya bado haimfanyi mdhambi ila si utaratibu na ndiyo maana kuna watu maalum kila Jumapili (wakiwa na utambulisho) hupewa hilo jukumu.
ASANTE MTUNGA MADA.
 
Hivi nyinyi binadamu hasa tanzania aliyewaroga amekufa au?
Mtoa mada mpumbavu.
Rais akiwa mkali mnalia,akiwa karibu na watu mnalia sasa mnataka nini.
Mimi hiyo sio dini yangu lkn naona hakuna kosa.
Hivi kuna mtu ameshushwa toka mbinguni anatakiwa kukusanya hizo sadaka?
Si ni binadamu tu wa kawaida.
Waumini kama wewe hamfai katika hiyo dini.
Acha utoto.
 
Daaah...mna chuki mpaka mnakuwa wajinga !
 
Hichi ulichoandika chini ndio duku duku lako lakini si hoja ya kuingilia utaratibu.
Ila bado hujajisaidia maana tafuta dini ya kweli, hiyo ni dini ya kupanga tuu !
 
Utaratibu wakukusanya sadaka niwakawaida nawanaokusanya sadaka niwaumini wakawaida
Kwahiyo kitendo alichokifanya Mh Raisi nichakawaida sana sana
Tena kwa nafasi yake nikitu kikubwa sana kumfanyia Mwenyenzi Mungu Mkuu
Mimi mkatoliki nileyesoma uchaghani useminarini nijambo zuri sana
 
Na jamaa yumo kwenye kikundi cha kwaya pia ! Jamaa wana chuki na nongwa mpaka basss !
 
Je alipangiwa kukusanya!? Hakuna cha chuki kama wajinga waliokunywa maji ya viatu wanavyodai. Ibada ziheshimiwe.
Kwahiyo sala /ibada haikuswihii ! ? (yaani sala /ibada haikukamilika kisa sadaka ?)
 
Nadhani una matatizo kichwani mwako. Dkt Magufuli kalelewa na wakatoliki anafahamu taratibu zote! Wewe utakuwa ni mkatoliki wa vyama vya upinzani, ukome kushobokea vitu visivyokuhusu.
@fisi 2 ni mkatoliki wa upinzani (make sense)
 
Sisi bwana akija Msikitini Sheikh Alhaj Ally Hassan Mwinyi (enzi akiwa Rais) ndio anakuwa Imamu (anaongoza sala)
 
Na we we pia kapanue ubongo,
Kufagia ama kusafisha siyo lituljia ni majitoleo,
Duuh....sadaka kumbe inaitwa 'liturjia' !
Wale walokole zile.za upaka, mafuta, sijui zaka, kufunguliwa hazifanani na liturjia
 
Duh kumbe wakatolik mpo makundi mawili
A-Wanaomshobekea Rais bila ya shaka wanaongozwa na PENGO
B-Wakatoliki wa upinzani hao kiongoz wao bado hamjatuambia
Askofu TLissu !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…