Rais Goodluck Jonathan aomba msaada

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,098
Reaction score
34,913


Serikali ya Nigeria inahitaji msaada wa dola billioni moja ili kukabilina na wanamgambo ambao wameliharibu taifa hilo katika miaka ya hivi karibuni.

Rais Goodluck Jonathan ametuma barua katika bunge la seneti ili kuidhinisha ombi hilo ambalo litasaidia kuimarisha vifaa vya kijeshi.


Zaidi ya watu 2000 wameuawa mwaka huu katika ghasia zilizosababishwa na wapiganaji wa Boko haram.


Huku umwagikaji wa damu ukiendelea Kazkazini mwa Nigeria ,rais Goodluck Johanathan anaendelea kupata shinikizo.


Kuna ripoti kwamba wanajeshi wengi katika vita vya kukabiliana na wanamgambo hao hawana vifaa vya kutosha na hivyo basi kushindwa kuwakabili waasi hao.


Ijapokuwa jeshi halijakiri kuhusu madai hayo linakubali kwamba linahitaji vifaa zaidi ili kukabiliana na vita hivyo.


Rais Goodluck Johnathan anasema kuwa kuna umuhimu wa kulinunulia jeshi vifaa zaidi ili kukabiliana na tishio la Boko Haram.

Wakosoaji hatahivyo wamelishtumu jeshi kwa utumizi mbaya wa raslimali zilizopo. Chanzo. BBC
 
A billion dollar kupambana na Boko haram, kwani hao jamaa ni jeshi kubwa namna gani? One billion dollar! Lakini kumbuka kuna uchaguzi mwaka kesho mkuu so maybe this is one way of getting them moneys for the election period!
 
It's another drama. Nigerian Defence forces asking for reinforcements to combat a group of terrorist within Nigerian borders!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…