Rai yangu kwa watawala wetu

Mushkov

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2024
Posts
671
Reaction score
1,407
Ndugu zangu watawala, huu utekaji, utesaji na mauaji vinavyoendelea kushamiri katika nchi hii vinaligawa Taifa letu kimakundimakundi.

Hali hii pia inajenga chuki katika Taifa. Mimi naomba watawala wetu wajitathmini kama wanatosha vizuri katika nafasi zao wakati jambo dogo tu hili linawashinda.

Siku watu wakiishiwa uvumilivu hali itakuwa mbaya zaidi. Wakati huo hakutakuwa na wa kumsikiliza mwenzie.
Wazee wastaafu, tokeni huko mafichoni, kemeeni jambo hili, maana mliobaki ni nyie.

TEC, CCT na wengineo wamesema mara kadhaa lakini WAMEPUUZWA.
 
Si wameshavikamata tayari vile vidagaa!! Au unataka wakamate pia samaki wakubwa wanaozituma hizo dagaa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…