Mtoboasiri
JF-Expert Member
- Aug 6, 2009
- 5,100
- 1,955
Jamani huyu ni mheshimiwa MBUNGE wetu.daah kumuona na kumsikilaza RAGE tu ni kati ya maajabu saba ya dunia
Jamani huyu ni mheshimiwa MBUNGE wetu.
Sunderland yaikana Simba
Na Mwandishi wetu
13th September 2013
Mkurugenzi wa Biashara wa Sunderland, Gary Hutchinson.
Uongozi wa timu ya Sunderland inayoshiriki Ligi Kuu ya England umesema hauna ubia wa ushirikiano na Simba licha ya uongozi wa klabu hiyo ya jijini Dar es Salaam kukaririwa mara kadhaa wakitamba kuwa na makubaliano ya ushirikiano na klabu hiyo ya Ulaya.
Akizungumza katika mahojiano maalum na NIPASHE jijini Dar es Salaam juzi, Mkurugenzi wa Biashara wa Sunderland, Gary Hutchinson alisema klabu yake haijawahi kuingia katika makubaliano ya ushirikiano na klabu yoyote ya Tanzania.
Hutchinson alisema uongozi wa Sunderland uko katika mazungumzo ya ushirikiano wa kibiashara, michezo na utalii na serikali ya Tanzania na kwamba hauna mpango wa kuwa na ubia na klabu yoyote ya michezo nchini.
Alisema kuwa kwa sasa barani Afrika Sunderland ina ubia na klabu mbili tu za Ghana na Afrika Kusini ambazo huzisaidia kwa kuzitangaza na kuzitafutia wafadhili na mawakala wa wachezaji.
"Ushirikiano ambao unaelekea kukamilika kwa sasa ni wa klabu yetu na serikali ya Tanzania baada ya kuombwa na Rais wa nchi hii (Jakaya Kikwete) alipotembelea uwanja wetu wa Stadium of Light Juni mwaka huu," alisema Hutchinson.
"Kwa sasa tuna ushirikiano na timu mbili za Afrika ambazo ni Asante Kotoko inayoshiriki Ligi Kuu ya Ghana na Bidvest Wits ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini, " aliongeza.
Mtandao wa klabu hiyo iliyotwaa mara mbili ubingwa wa FA pia unazitaja Asante Kotoko na Bidvest Wits kuwa ndizo timu pekee kutoka barani Afrika zinazofadhiliwa na Sunderland.
Mei mwaka huu viongozi kadhaa wa Simba walikaririwa wakidai kuwa wamemshawishi mmiliki wa Sunderland, Ellis Short kukubali kuisaidia klabu yao.
Viongozi hao walidai kuwa uongozi wa klabu hiyo iliyoanzishwa 1879 umekubali wachezaji kupata nafasi ya kufanya majaribio Sunderland, makocha wao kupewa mafunzo na kujengewa kituo cha soka (academy) na uwanja wa mazoezi kwa timu za Simba za vijana.
Alipotafutwa na gazeti hili jijini Dar es Salaam jana kuzungumzia suala hilo, Msemaji wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema uongozi wa juu wa Simba ndiyo uliokwenda kuzungumza na uongozi wa Sunderland lakini bado hajaelezwa chochote juu ya yaliyozungumzwa Uingereza.
Klabu ya Simba ambayo ilianzishwa 1936 ilikuwa ikijulikana kwa jina la 'Sunderland' lakini baadaye lilifutwa kufuatia tamko la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere lillilotaka kufutwa kwa majina ya 'kizungu' katika klabu zote za michezo nchini.
My Take:
Haya wapenzi/wanachama wa Simba muulizeni Rage awambie vizuri. Ni Sunderland gani hiyo aliyotutangazia kuwa ina ushirikiano na Simba?
Huyo Mama sio kiongozi wa Simba labda walikutana kwa mambo yao binafsi au ya kibiasharaHii ni habari ya Feb 13, 2013. Nanukuu . . . . .
Pichani ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ya Simba, Rahma Al Kharusi akiwa na Mwenyekiti wa Sunderland ya England, Ellis Short baada ya kukutana kwenye hoteli ya Hayat jijini Dar es Salaam.
Baada ya kukutana, wawili hao walijadili kuhusiana na klabu hizo mbili kuanzisha uhusiano wa kibiashara pamoja na mafunzo na Simba imepata mwaliko.
Malikia wa Nyuki ataiongoza Simba nchini England mwezi Machi 2013 ambako watatembelea viwanja vya Sunderland ikiwa ni pamoja na kujifunza uendeshaji wa klabu, SASA NANI TAPELI HAPO RAGE AU HUYO MWENYEKITI WA SUNDERLAND PICHANI?? AU NDO ILIKUWA GIA YA KUINGILIA SERIKALINI KUPITIA MGONGO WA SIMBA, SUNDERLAND NI KLABU YA MPIRA NI URAFIKI GANI INAANZISHA NA SERIKALI BADALA YA KUANZISHA NA VILABU VYA SOKA??
Hii ni habari ya Feb 13, 2013. Nanukuu . . . . .
Pichani ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ya Simba, Rahma Al Kharusi akiwa na Mwenyekiti wa Sunderland ya England, Ellis Short baada ya kukutana kwenye hoteli ya Hayat jijini Dar es Salaam.
Baada ya kukutana, wawili hao walijadili kuhusiana na klabu hizo mbili kuanzisha uhusiano wa kibiashara pamoja na mafunzo na Simba imepata mwaliko.
Malikia wa Nyuki ataiongoza Simba nchini England mwezi Machi 2013 ambako watatembelea viwanja vya Sunderland ikiwa ni pamoja na kujifunza uendeshaji wa klabu, SASA NANI TAPELI HAPO RAGE AU HUYO MWENYEKITI WA SUNDERLAND PICHANI?? AU NDO ILIKUWA GIA YA KUINGILIA SERIKALINI KUPITIA MGONGO WA SIMBA, SUNDERLAND NI KLABU YA MPIRA NI URAFIKI GANI INAANZISHA NA SERIKALI BADALA YA KUANZISHA NA VILABU VYA SOKA??
Naogopa kutolewa nje na naibu wa spika.Unatakiwa kusema "Mheshimiwa MBUNGE MUONGO!"
Huyo Mama sio kiongozi wa Simba labda walikutana kwa mambo yao binafsi au ya kibiashara
Lakini mazungumzo ya ushirikiano kati ya Simba na Sunderland yalianzishwa na JK hapa Dar wakati viongozi wa Sunderland walipomtembelea Ikulu, na mwishowe Malkia wa Nyuki na Rage wakapewa mwaliko wa kwenda makao makuu ya Sunderland. Waliporejea nchini ndo Simba ikaanza kutumia jezi kama za Sinderland.
Nadhani hawa Sunderland wamegeuza kibao baada ya JK na wale warithi wa Dowans kutembelea makao makuu ya Sunderland, na nahisi kuna mchongo umepigwa baada ya ziara hiyo ndo maana jamaa wanaikana Simba na kujifungisha ndoa na Tanzania.
Huu ni urafiki gani kati ya nchi na klabu tu ya mpira ambayo uchumi wake na kiwango chake cha soka si mkubwa sana?
Na kwa kuthibitisha michongo imeanza, tangu July pale Stadium of Light kuna matangazo ya hifadhi zetu.