Kitendo cha madreva kugoma, ni atua nzuri inayoonyesha wametambua haki zao sasa kwa mujibu wa sheria za nchini zinavyotaka.
Madreva wamekuwa wakifanya kazi kwenye mazingira magumu kulingana na manyanyaso wanayopata kutoka kwa waajiri wao, wengi wanalipwa mishahara mibovu, mikataba ya kazi hawana, bima ya afya hawana, hata likizo hawapewi; sasa madreva baada ya kuligundua hilo hasa mara baada ya Elimu nzuri inayotolewa na Maafisa Kazi kutoka Wizara ya Kazi na Ajira juu ya sheria za kazi, na wao kutambua ni wapi wanapunjwa na kwa vile waajiri hawataki kubadilika basi matokeo yake ni Kugoma kwani ni Haki yao kisheria.