QUR'AN

Zerock

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2026
Posts
1,001
Reaction score
2,025
1: Sifa njema zote ni za mwenyezi Mungu aliyeumba mbingu na ardhi, na akafanya giza na mwangaza. Tena baada ya haya waliokufuru wanawafanya wengine sawa na mola wao mlezi.

2: Yeye ndiye aliyekuumbeni kwa udongo,kisha akakuhukumieni ajali, na muda maalumu uko kwake tu. Tena baada ya haya nyinyi mnatia shaka.

3: Na yeye ndiye mwenyezi Mungu mbinguni na ardhini, anajua ya ndani yenu na ya nje yenu, na anajua mnayoyachuma

4: Na haiwafikii hata ishara moja katika ishara za mola wao mlezi ila wao huwa wenye kuipa nyongo.

5: Wameikanusha haki ilipowajia, Basi zitawajia khabari za yale waliyokuwa wakiyakejeli.

6:Jee hawaoni vizazi vingapi tulivyoviangamiza kabla yao?
Tuliwaweka katika nchi tusivyo kuwekeni nyinyi ;tukawapelekea mvua nyingi na tukaifanya mito inapita chini yao. Mwisowe tukawaangamiza kwa madhambi yao;na tukaanzisha baada yao kizazi kingine.

7: Na lau tungeli kuteremshia kitabu cha karatasi wakakigusa kwa mikono yao, wangeli sema waliokufuru: Haya si chochote bali ni uchawi dhahiiri.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…