Baadhi ya Waafrika ni watu wa ajabu sana! Wanapenda kuikuza historia potofu, inayowafanya waafrika kuonekana kama si watu kamili, hawajui chochote na hawakuwa na historia yenye ustawi kwa jamii yao ya kale! Hii ni historia iliyoandikwa na watu wasio waafrika. Lengo lao kutaka kuitawala jamii nyingine kifikra.
Kila jamii hapa Duniani ilikuwa na ustawi na maendeleo yake na mfumo kamili wa kujiendesha! Ndio maana tupo. Kama tungekuwa ni jamii yenye mapungufu, tusingeweza kuwepo katika uso wa dunia.
Ni upumbavu wa kiakili kutafuta kuhalalisha kuwa jamii moja ilikuwa bora zaidi ya nyingine! Jamii zote zilikuwa sawa, na kila moja ilikuwa na ustawi na maendeleo yake kulingana na mahitaji ya wakati na mazingira.
Ninarudia tena, ni upumbavu wa kiakili kutaka kuhalalisha kuwa, jamii moja ilikuwa bora kuliko jamii nyingine. Jamii ya wafugaji haiwezi kuwa bora zaidi ya jamiii ya wakulima; jamii ya wakulima haiwezi kuwa bora zaidi ya jamii ya wavuvi; na jamii ya wafugaji, wakulima ama wavuvi haiwezi kuwa bora zaidi ya jamii ya wawindaji. Haya ni mazingira tofauti, na mahitaji tofauti kwa wakati tofauti.
Hivyo, jamii ya waarabu kama unavyotaka kuhalalisha hoja yako, haikuwa bora zaidi ya jamii ya wachina, waafrika, wahindi na hata wazungu. Hilo linawezekana tu kwa mazuzu wa akili wasiotaka kujielimisha na kujua histori ya nzuri ya jamii yao. Lakini kutaka kulinganisha ustawi wa jamii moja kwa kutegemea historia ya jamii nyingine, huoni upumbavu wa kiakili uliopindukia mipaka.
Hiyo nisawa na kujifunza historia ya Tanzania kwa kusoma historia iliyoandikwa na mtu asiye mtanzania, na hajawahi hata kufika au kuishi au kuwaona watanzani! Utaishia kupoteza hata kidogo ulichokijua kuhusu Tanzania.
Kwa hiyo, jamii moja haiwezi kuwa kipimo cha ustawi na maendeleo kwa jamii zingine. Mwisho wake ni kuishia kutukuza jamii nyingine na kudharau jamii yako. Utumwa uliovuka mipaka.