Protein ikionekana kwenye mwilini ina madhara

miss strong

JF-Expert Member
Jul 4, 2012
7,012
3,694
Habar zenu wana jamvi.......
Kuna tatizo ambalo linanitatiza mwenzenu,mwili wangu unakawaida yakuwa na joto maisha yangu yote kias ya kwamba mtu mwingine akinigusa anaweza akasema labda naumwa kumbe walaaaaah!!!

Kilichonifanya niandike uzi huu....nilipotoka kijiji hv karbun nikawa najisikia vbaya kias.Leo ikabid niende zangu hosptl nkapime malaria,u.t.i,typhod lkn vipimo vmeonyesha nna malaria 2 na hvyo vingine sina ila pia imeonyesha protein nying.Je protein hii inaweza ikaleta matatizo???au ni inakuaje??

Mungu awabariki sana....nategemea michango yenu wote na MziziMkavu, Dr.Mo, King'asti, mimi49
 
Last edited by a moderator:
Mimi sio daktari, lakini nafahamu kuwa protein haitakiwi kuwepo kwenye mkojo. Mara nyingi ikiwepo inaashiria matatizo ya figo. Poleeh!
 
Could it be an infection? Mi najua inakuwaga issue unapokuwa mja mzito but tusubiri wenye info zaidi.
 
Protini



Protini ni molekuli ndefu na sehemu za lazima katika muundo wa seli za mwili wa viumbe hai.

Zinajengwa na amino asidi. Protini huwajibika kwa maumbile ya seli na kushughulika usafirishaji

wa dutu ndani ya seli na kati ya seli za mwili. Musuli zinaundwa pamoja na protini za pekee zenye

uwezo wa kupanua na kujikaza hivyo kuweka msingi wa mwendo.



Protini zinapatikana katika wanyama, mimea, fungi na bakteria.



Protini katika chakula

Wanyama wote pamoja na binadamu huhitaji protini katika chakula chao kwa sababu hawana

uwezo wa kujijengea amino asidi zote zinazohitajika kwa kujenga miili yao. Kwa sababu hiyo

tunahitaji chakula chenye protini; mahitaji ya mwanadamu ni takriban gramu 1 ya protini kwa

kilogramu 1 ya uzito wa mwili wake; maana mtu mwenye uzito wa kilogramu 70 anashauriwa kula

gramu 70 za protini kwa siku.


Tumboni mwa binadamu na wanyama protini za chakula huvunjwa kwa asidi asidi ndani yao;

kutoka hizi mwili unajenga protini mpya ya aina yake ya pekee.


Uhaba wa protini unasababisha magonjwa; uhaba mkali unaleta unyafuzi. Unyafuzi unashika hasa

watoto wanaopewa chakula kingi lakini kabohidrati tu kama ugali bila makundekunde, nyama au

samaki.


Vyakula vyenye protini nyingi ni



Protini ni muhimu kwa kulinda wewe mwili wako na Maradhi ikiwa wewe huna

matatizo ya Maradhi ya Figo sioni ubaya kuwa na Protini nyingi mwilini mwako. Ila

ukitaka kupunguza Protini Mwilini punguza hivyo Vyakula vinavyozidisha Protini

mwilini navyo hivi hapa chini.cc.@
miss strong

Vyakula vyenye protini nyingi ni

 
Kwani daktari amekuambia kutokana na kipimo chako hio protein ni kiasi gani yaani two digits number?
PROTEINURIA ni tatizo la wingi wa protein kwenye mkojo ambao huzidi(30-50mg/day)ambacho ndio kiwango cha kawaida!
Proteinuria imegawanyika katika makundi tofauti:
  1. Microalbuminuria 300mg/day
  2. Low proteinuria 300mg - 2g/day
  3. Moderate proteinuria 2g - 5g/day
  4. High proteinuria over 5g/day
Wingi wa protein mwilini unasababishwa na mambo tofauti nayo ni
  • Matatizo kwenye mafigo aidha inflammation(Glomerulonephritis) au infection kwenye mafigo na mirija ya mkojo,aina hii ya infection kwenye mirija ya mkojo inaweza kusambaa mpaka kwenye mafigo ambapo mkojo unakuwa filtered/kusafishwa...Hali hii husababisha mafigo kutoweza kufanya kazi ipasavyo na kupungua kwa uwezo wake wa kusecrete maji na wastes nyingine!
  • Unaweza kupata tatizo hili kama complication ya ugonjwa wa kisukari kwa wale walouugua muda mrefu au
  • High blood pressure/presha ya muda mrefu
  • Orthostatic proteinuria ni tatizo linalowapata watu wengi ambalo linasababishwa na leakage ya protini kutoka kwenye mkojo haswa wakati wa siku.Watu hawa wana production ya mkojo ya kawaida usiku kwamaana hio hakuna protini kwenye mkojo wa mwanzo wa asubuhi.Hali hii inaweza kuwapata asilima 3-5 ya watoto na wakubwa na haina madhara yoyote na haihitaji tiba yoyote.
Nakushauri uende tena ukapime kipimo cha mkojo,na muhimu upime mkojo wa mwanzo wa asubuhi unapoamka!
 
Habar zenu wana jamvi.......
Kuna tatizo ambalo linanitatiza mwenzenu,mwili wangu unakawaida yakuwa na joto maisha yangu yote kias ya kwamba mtu mwingine akinigusa anaweza akasema labda naumwa kumbe walaaaaah!!!

Kilichonifanya niandike uzi huu....nilipotoka kijiji hv karbun nikawa najisikia vbaya kias.Leo ikabid niende zangu hosptl nkapime malaria,u.t.i,typhod lkn vipimo vmeonyesha nna malaria 2 na hvyo vingine sina ila pia imeonyesha protein nying.Je protein hii inaweza ikaleta matatizo???au ni inakuaje??

Mungu awabariki sana....nategemea michango yenu wote na MziziMkavu, Dr.Mo, King'asti, mimi49
....pole sana kwa tatizo lako mamy. miss strong...kwa kuaangalia haraka haraka...joto mwilini linweza keletwa na vitu vingi...kama hivyo ulivyopimwa hapo....na hilo la kuwa na protein nyingi mwilini sina hakika na hicho kipimo walichotumia...maana si rahisi kujua wingi wa protein mwilini(kibongo bongo) japo unaweza kuona protein kwenye mkojo na inaweza kuwa ni kwa sababu ya magonjwa mengine.(maana kwa kawaida hutakiwi kuon protein , sukari kwenye mkojo)...tukirudi kwenye joto mwilini ukiacha mambo menginee makubwa labda kwa haraka harak ujiangalie pia km apetite ya kula ipo juu yaani ukila kidogo unapata njaa baada ya muda mfupi, km wakati mwingine moyo huenda mbio sana(palitation), au unakua unapata loose stool mara kwa mara....kama utakua na baadhi ya hizi dalili...uende hospital ukapime thyroid hormone(Thyroid function test).....lakin ukukikutana na dr ukiongea nae vzr ataangalia vitu vingine vinavyo sababaisha.joto kuwa juu..hasa hormone zinazishughulika na utengenezaji wa nishati kwa mwili( zinazo control Basal metabolic rate-BMR)..ila baada ya kuangalia all infections kama ulivyopima..
 
hata mimi tatizo kama hilo nilinitokea, proten ilizidi nywenye mkojo na hii inatokana na kwamba sinywi sana maji...ila nimejirekebisha na mara ya pili nilivyorudi hosp. Ikawa imeisha...NB kunywa maji mengi sana maji ni tiba
 
Back
Top Bottom