Prof. Mwandosya anena ya moyoni

Status
Not open for further replies.

usimungunye maneno utapasuka tumbo.mwandosya hamkubali magufuli hata chembe
 
"tumeyumba turudi katika misingi. Itikadi ya Chama inajengwa juu ya misingi hiyo. Hivyo basi kwangu mimi Ilihali misingi ipo, na imara, nitaendelea kuwa mwanachama wa CCM ili kwa pamoja na wanachama wenzangu tuendelee kulijenga Taifa juu ya misingi hiyo, kila wakati tukikumbuka kile alichotuasa Baba wa Taifa, Tujisahihishe!" By Prof. Mwandosya

Mzee anajua kuwa ,misingi ilishapotea,ccm ni skeleton , wamebaki waporaji wa Democrasia
 
Uoga na unafiki ndio umemtawala..... Ingawa nafsi yake anatamani kutoka

Mkuu Ocampo Four ...... umepotea na zile thread zako Kabla na wakati wa "hakatwi au Anakatwa" hope zinaendelea na Part II.:whoo:
 
ur real de prof even ur speech determines ow critical thinker u r bt ccm is no longer now days
 
Proff umeongea vitu vya msingi sana soo touching, lkn kwa upepo unaovuma sasa sidhani kama Ccm itabaki madarakani mtajisahihisha mkiwa chama pinzani.
 
Nimegundua kwamba ni dhahiri Prof.Mark Mwandosya hamkubali Magufuli na haoni kama atamudu kukiimarisha chama hata kama ataukwaa urais

Ni katika wanafiki, waoga, wasiojiamini, kwanini alisita kusema hayo mara tu baada ya kukatwa mpaka apitie mgongoni kwa Lowassa.
 

Sasa mbona unaongea mafumbo mafumbo tu ndugu....sema neno moja tukuelewe...watanzania wengi hawana elimu ya level yako...au umewajibu maprofessa wenzako???
 
Rasimu ya Katiba ya Tume chini ya Jaji Warioba ndio ilikuwa fursa ya KUJISAHIHISHA.

Lakini kwa sababu kitengo wanataka kuendeleza kusaini mikataba ya dharura, kupitishwa sheria za kutishia wananchi kwa ghafla ghafla bila kutaka mahojiano.
Ni dhairi CCM madikteta na hilo tuliona kwa mara nyingine hata ktk kupitisha Rasimu ya Samwel Sitta iliyojaa vipengele vya kulinda maslahi ya viongozi ambayo mtakumbuka ilihaririwa kikamilifu na mkongwe Andrew Chenge ili tuipigie kura ya ndio kama watakavyo chama cha zamani.

Hakuna fursa tena KUJISAHIHISHA wakiwa madarakani, tunataka nanyi mje kuwa raia ndio mtaonja machungu ya sheria za kulinda watawala
 
Kwa hali ilivyo, ni bora ccm ingetafuta kujua idadi ya wapinzani ndani ya ccm waliotokana na maamuzi tata ya Dodoma.

Kwa maelezo ya prof naweza kuamini yeye ni mmoja wao. Haamini kama uteuzi uliofanyika ulizingatia uhalisia.

Swali, je wengine ni kina nani? Maana ni heri kama wapinzani watahama chama kwa kuwa unaweza kukokotoa idadi ya kura zilizopotea. Wanaobaki ndani ya chama ni kama kansa, na ndio hatari zaidi kwa ustawi wa chama.
 
Uoaga ni kitu kibaya sana! Yaani mtu mzima na heshima zake anashindwa kuwa wazi kuongea na kueleweka? Amemung'unya maneno mno, na hii sio "busara" ni uoga na ubinafsi (wa kuendelea kufikiria tumbo lake) tu!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…