Asante Prof Mwandosya kwa busara zako. Lakini ni misingi ipi unayoongelea juu ya chama chenu ambayo iliwekwa na hao waasisi uliowataja ambayo bado ipo hai (valid )? Ni kweli wapendwa hao waasisi waliweka misingi safi na imara, ambayo mara walipotoweka ilikosa wa kuilinda na hivyo ikatoweka. Prof kama ulikuwa huna habari hivi sasa misingi hiyo imebakia historia tu. Sana sana wewe na baadhi ya wenzako mnadanganywa tu kwamba bado mpo ndani ya misingi hiyo. Na ninashauri msiendelee kutumia majina ya hao waasisi kwa lengo tu la kufanikisha masilahi yenu, huku miiko waliyoiamini mmeiacha. Asante.