Prof. Mark Mwandosya ni mpotoshaji

Katibiwa siyo msaada ni haki yake kama vile mtu baada ya kustaafu anapewa pension yake na pension inategemea ulikuwa kwenye nafasi gani. Wengine mpaka usafiri wanaendelea kupata nk
 
Jipe moyo
 
Comparison ya kijinga kabisa. Hivi michakato ndani ya CCM kupata mgombea iwe urais, ubunge, udiwani au upuuzi mwingine ni kipimo cha uadilifu wa wahusika? Are you serious? Prof. Mwandosya jina lake kutopitishwa kugombea urais haina maana kuwa hana akili, au sio mwadilifu kulinganisha na waliopitishwa. Na Chadema hawajamuita Prof. Mwandosya kutoa maoni yake kuhusu kuachiwa Sugu. Ametoa maoni yake kutimiza haki yake ya msingi. Na sijui kwanini ugonjwa wa kuchukia watu wanaokuwa na maoni msiyoyapenda unaongezeka kwa kasi ya namna hii!
 
Sawa, unaweza kutuambia ni matusi gani hayo? Sugu alifungwa kusiasa na ndio maana hata kutoka kwake kulikuwa ni kwa kisiasa. Iweje wampeleke nyumbani kwake kimya kimya? Ina maana Sugu alisahau njia ya kwenda home. Mbona kina Papii Kocha hawakupelekwa home na polisi?
 
Hata mimi nashangaa kwa nini SUGU alihamua kumdhihaki Mh. Rais wetu
 
Halafu unaweza kuwa ni graduate wa moja ya vyuo vikuu vya "mwendo-kasi". Hivi ulishawahi kuona kwenye penal code kuna kosa la jinai linaloitwa "kosa la kisiasa" ambalo baadaye kupitia kosa hilo anapatikana "mfungwa wa kisiasa", kiasi cha kuanza kuwashtumu, kupitia makala ndefu kama hiyo, wale wanaosema kuwa Sugu "alifungwa kisiasa" akiwemo Profesa Mwandosya?
 
Huyo mzee Kuna kitu anakitafuta maanake hajaanza Leo huko kujifaragua.

Ni muda tu atakipata akitakacho SI juzi Tu alidai hii awamu imemsahau? Watamkumbuka Tu yeye akomae kutafuta attention.
 
Nakumbuka vizuri sana baadhi ya mambo makubwa alofanya Mwandosya enzi za uwaziri as mawasilianao na uchukuzi.
Huyu ndiye aliyewaleta wale Wafaransa TTCL. Baadae wakaanzisha Celtel kwa gharama na Rasilimali za TTCL
. Kisha wakaiua TTCL wakabaki na CELTEL. Famous na mengine wake maana delineates Mwandosya scholarship ya binti take.
Leo hii tunazungumzia kuirudisha Airtel serikalini kwa madudu ya Mwandosya. Unafiki katika siasa hautokoma kamwe.
 
balaaaaaaa kubwa sana..................umetoa makavu live
 


Hacha upotoshaji wewe hakuna mtu mfungwa wa kisiasa ambaye anafungwa bila kutenda kitendo au kusingiziwa kutenda kitendo ambacho ni kinyume na sheria za nchi husika. Nelson Mandela na wenzake 7 walifungwa kwa kukutwa na hatia ya kuvunja Kifungu vya sheria zifuatazo;

(1) Section 21 (1) cha the Sabotage Act, 1962 (Sheria Na. 76 ya 1962);
(2) Sections 1,12 and 11(a)The Suppression of Communism Act, 1950 (Sheria Na 44 ya 1950)
(3) S. 2 of Criminal Law Amendment Act, 1953 (Sheria Na 8 ya 1953)

Hivyo wafungwa wa kisiasa nao ufungwa kwa visingizio vya kuvunja sheria za nchi, hakuna, kama ilivyo kuwa kwa Mandela na wenzake wakina Susulu, Mbeki (Govan),Mlangeni n.k ndivyo ilivyo kwa kwa Mzee Kenyatta ambaye alihukumiwa kwa kuvunja Section 71 and 72 of Penal Code. Hivyo basi, wafungwa karibu wote maarufu ambao historia inawaita wafungwa wa kisiasa ufungwa kutokana na kinachoitwa kuvunja sheria na kwa wakati huo uonekana ni waharifu machoni mwa sheria na utawala wa wakati husika na pia upewa namba za mfungwa kama alivyopewa Sungu hata Mandela alikuwa mfungwa namba 220/82. Hivyo, hoja zako dhaifu haziondoa hadhi ya Sugu kuwa mfungwa wa kisiasa iwapo anastahili kuwa na hadhi hiyo. Swala mtu kuwa ni mfungwa wa kisiasa kwa kawaida sio swala la kisheria bali ni swala la kisiasa na kijamii, swala huwa jamii inatizamaji kifungo hicho, iwapo itakiona ni kifungo cha kijinai basi mfungwa ataonekana kama mharifu na kama jamii itakiona ni cha kisiasa mfungwa ataonekana ni shujaa.
 
Nilikuwa nimekosa imani na Maprofesa na Madaktari (PHD) angalau mzee Mwandosya amejitenga na Maprofesa uchwara.
 
Wewe unaejiita Jumanne, ulitaka Mwandosya aandike nini ili ufurahie, kama unaona ni uchochezi kwa mujibu wa katiba unaweza kufungua mashitaka,
 
Hivi hua mnapata wapi muda wa kujibu utumbo kama huu mkuu? Yaani mtu ambaye hata hajui ni wafungwa gani duniani waliwahi kufungwa halafu mahakama zikakiri kua ni makosa ya kisiasa, mnapoteza muda mujibu upuuzi. Binafsi sinaga muda huo. Nani aliwahi kufungwa halafu mamlaka zikakubali kua ni mfungwa wa kisiasa? Wanasiasa hufungwa kwa kwa visingizio vya kuvunja sheria. Sasa hapa mtu anatokwa povu halafu hajui anachoandika. Shule zetu za kata hizi zimeharibu watu sana kwa kukosa walimu wa kuwaelimisha
 
Lumumba kwa mahangaiko hawajambo ,sasa hapo kuna kosa gani?
Njaa zitawaua nyie maana bila hivi vipost mshenzi vyenu hamli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…